Benki ya NCBA imesisitiza dhamira yake ya kuwawezesha wanawake zaidi kupitia uvumbuzi wa kifedha ili kukuza ari yao ya ujasiriamali na biashara. Ahadi hiii ilitolewa Machi 26 kwenye hafla ya kuwapongeza Wanawake kwenye uongozi, maarufu kama Women in Management (WIMA).
Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya NCBA, Margaret Karume alikuwa miongoni mwa wanawake waliotunukiwa tuzo ya heshima kwenye hafla hio alikaririwa akisema, "uwezeshwaji wa wanawake kwenye kazi zao ni kipaumbele chetu, iwe ni kwenye biashara, ujasiriamali au kazi za kawaida. Hii ni kwasababu benki yetu ina uwezo mkubwa wa kifedha, uwekezaji, na uvumbuzi hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kuwa kama mhamasishaji, msaidizi, muongozaji, na mshirika wao kwenye kila hatua zao za mafanikio’.
Sambamba na hayo, benki ilitoa wito wake kwa wadau wengine kudumisha na kurekebisha mifumo endeshi ili kupunguza tofauti ya kipato kati ya wanaume na wanawake katika kuleta ushirikishwaji wa wanawake kwenye sekta rasmi ya fedha.
Kwa mujibu wa Gloria Njiu ambae ni Mkuu wa Biashara za Kidijitali wa Benki hio alisema, ‘sisi kama taasisi wa huduma za fedha ni lazima tuwe wabunifu zaidi ili tuwajumuishe wanawake zaidi katika mfumo rasmi wa fedha. Tunahitaji kuweka miundombinu thabiti na rafiki itakayowawezesha wanawake zaidi kunufaika na fursa hizi’.
Gloria alitolea mfano wa huduma yao ya M-PAWA ambayo imewezesha watanzania takribani milioni kumi kupata mikopo ya haraka, hivyo kuwajumuisha pia wanawake wengi zaidi kwenye mfumo rasmi wa fedha.
Benki ya NCBA ni mojawapo ya benki kubwa zaidi kwa idadi ya wateja barani Afrika ikiwa na wateja zaidi ya milioni 40 kote barani Afrika. Ni benki yenye nguvu kifedha, utaalamu, uhudumiaji mpana wa kukidhi matarajio ya wateja nchini na kusaidia ukuaji wa kiuchumi. Benki ya NCBA kwa sasa ina matawi 12 nchini Tanzania katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa NCBA Bank, Margaret Karume (katikati) akiwa na Caroline Mbaga, Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uraia wa NCBA (kushoto) na Mansoor Baragama, Mkuu wa Rasilimali wa NCBA (kulia)Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa NCBA Bank, Margaret Karume akiwa na tuzo yake kutoka WIMA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...