· Asema bidhaa zinakidhi viwango vya kimataifa

· Ataka zijazwe kwenye supermarket nchini

Na Mwandishi Wetu.


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo amepongeza maonyesho ya wafanyabiashara wanawake yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Waziri Jafo ametoa pongezi hizo leo Machi 5, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akifungua maonyesho hayo ambayo ya wanawake ambayo yanatarajiwa kufikia kilele siku ya Almahisi ijayo kwa wanawake mbalimbali kupewa tuzo.

Maonyesho hayo yameandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake (TWCC) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani GIZ na wafadhili mbalimbali.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo, Waziri Jafo amesema baada ya kutembelea mabanda mbalimbali amejionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wafanyabiashara wanawake ambazo nyingi zinaviwango vya kimataifa.

“Nimefarijika sana kuona bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na nyingi zina nembo ya ubora wa Shirika la Viwango TBS zinahadhi ya kuuzwa kwenye maduka mbalimbali makubwa hapa nchini mnastahili pongezi kubwa sana,” amesema

Amesema wanawake hao wameonyesha ujasiri wa hali ya juu kuanzisha vikundi vya uzalishaji bidhaa mbalimbali hali ambayo imechangia kuongezeka kwa nafasi za ajira kwa vijana, anawake na hata kwa wanaume wengi nchini.

Amesema pamoja na janga la ugonjwa wa COVID uchumi wa Tanzania umeendelea kufanya vizuri na wanawake wametoa mchango mkubwa sana kwenye kutengeneza fursa za ajira kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kimataifa.

Amesema amefarijika sana kuona wanawake wakiwa kwenye vikundi mbalimbali vilivyopata mikopo ya asilimia 10 zinazotoka kwenye halmashauri mbalimbali na kufanikiwa kuanzisha biashara zao ambazo zinakwenda vizuri.

“Kuna mabanda nimepita wameniambia wanauza bidhaa ndani nan je ya nchi hongereni sana kwa hatua hii kubwa mliyopita mafanikio haya tuliyofikia ni sababu ya wanawake kuwa mahiri ya kurejesha mikopo kwa wakati,” amesema Waziri Jafo.

Amesema anatamani sana kuona bidhaa hizo zinasambazwa kwenye maduka yote makubwa hapa nchini na zingine kusafirishwa nje ya nchi kwani zinasifa ya kuvuka mipaka ya Tanzania.

Aidha, Waziri Jafo amewataka wanawake hao kutumia fursa ya ujenzi wa miradi mikubwa kama ule wa kuzalisha Megawati 2,150 wa Julius Nyerere kwenda kuuza bidhaa zao kwa watu wanaofanyakazi kwenye mradi huo.

“Wakina mama nawaomba sana msiwe wanyonge nyinyi ni mashujaa kwa sababu nyinyi ndiyo mnajenga msingi wa nchi hii na mchango wenu kwenye maendeleo ya nchi ni mkubwa sana. Tuendelee kufanyakazi tumsaidie rais wetu kutimiza ndoto zake za kujenga uchumi imara,” amesema Jafo.

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Selemani Jafo akinunua shati kutoka kwa mjasiriamali kwenye maonyesho ya wajasiriamali wanawake yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake (TWCC)

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Selemani Jafo akisikiliza maelezo kutoka kwa mjasiriamali Betty Mkwasa alipokuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho ya pili ya wajasiriamali wanawake yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wanawake (TWCC), yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam



Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Selemani Jafo akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali wanaoonyesha bidhaa zao kwenye maonyesho ya pili ya wajasiriamali wanawake yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wanawake (TWCC), yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Selemani Jafo akifurahia jambo na Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake (TWCC), Mwajuma Hamza na Mwenyekiti wa chama hicho, Mercy Sila alipowasili kwaajili ya kufungua maonyesho ya pili ya wafanyabiashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...