Na Janeth Raphael 

Ikiwa bado ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)

umeitaka jamii kuhakikisha Wanasaidia makundi maalum kwa kuweza kuwapatia mahitaji mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza Jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa UCSAF Justina Mashimba katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya akili Mirembe walipokuwa wakitoa msaada kwa wenye mahitaji maalumu amesema kuwa ni muhimu kurudisha katika jamii kile ambacho unakipata hasa kwa makundi maalum yasiyojiweza

"Sisi kama kundi la wanawake tumeamua kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa hawa kwa umoja wetu kwakua mwezi huu niwa wanawake tumeamua kurudisha kwa jamii yenye uhitaji kwa kutoa vitu mbalimbali viweze kuwasaidia,"- Amesema

Justina amesema Jamii imetakiwa kutupia macho kwa taasisi zinazojihusisha na ulezi wa makundi maalum ikiwa ni pamoja na zile zinazohudumia wagonjwa wa akili.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt.Paul Lawala amesema  kuwa kundi la wenye ugonjwa wa akili linatakiwa kuangaliwa kwa umakini mkubwa hivyo jamii isiwatenge watu hao kwa kuwaacha pekeyao.

"Watu wenye ugonjwa wa akili mara nyingi huwa wanasahaulika katika jamii,muhimu tuwakumbuke na wao tusiwaache katika kuwapatia mahitaji mana wanatakiwa kupata huduma kama wengine,"amesema.

Naye Afisa Rasilimali watu UCSAF Adeline Kakoko amesema kuwa wameamua kuwa mfano kwa Kutoa kile walichonacho kwa kuanzia katika Hospitali hiyo ili kuweza kurudisha kwa jamii.

"tumeamua kutoa kidogo tulichonacho kwa jamii ili hata wanaoguswa wengine pia nawao waweze kupata hamasa ya kusaidia jamii hasa wenye mahitaji maalumu,"alisema.

Kila ifikapo tarehe 8 Machi ya kila mwaka wanawake Duniani wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali kwenye jamii ili kuweza kutumia maazimisho ya siku hiyo, Lengo kuu la siku hiyo ni kusherekea haki zilizopatikana kwa bidii za wanawake na kuangalia changamoto bado ziko mbele yao katika kukomesha ubaguzi wa kijinsia kwenye nyanja zote za maisha.

Baadhi ya misaada iliyokabidhiwa hospitalini hapo
Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Justina Mashiba (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirenbe Dkt Paul Lawala aliyeko  (katikati)
Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Dkt Paul Lawala






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...