"Kufuatia uwekezaji wa hivi karibuni wa Smile Tanzania katika upanuzi wa mtandao, tunayofuraha kuleta huduma bora zaidi za mtandao wa 4G LTE kwa wateja wa Zanzibar" Alisema Zuweina Farah Meneja Nchini Tanzania.
Uzinduzi huu umembatana na uwepo wageni kutoka sekta mbalimbali, waliohudhuria uzinduzi huu, Mgeni Rasmi Ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais anayeshughulikia Uchumi na Uwekezaji Mhe.Mudrick Soraga.
Smile imewekeza katika kusanifu upya na upanuzi wa mtandao
wake ili kuwapa wateja huduma zilizoboreshwa za intaneti zenye kasi ya haraka
zaidi ya data. Ukuaji wa wateja wa Smile katika kipindi cha miaka miwili
iliyopita umekuwa mzuri sana, kwani inaendelea kutoa mtandao wa kasi wa hali ya
juu na unaotegemewa kwa wateja na sasa wa Zanzibar, wateja wanapata uzoefu huo.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, huku Bi. Zuweina
Farah akishikilia Uongozi. Smile imewekeza katika kuunda upya na kupanua
mtandao wake ili kuwapa wateja huduma zilizoboreshwa za intaneti zenye kasi ya
data zaidi. Ukuaji wa wateja wa Smile umekuwa chanya sana, kwani inaendelea
kutoa mtandao bora na unaotegemewa wa uharaka zaidi kwa wateja.
"Tunafuraha kwamba watu wanaoishi, na wanaotembelea Zanzibar sasa watapata mtandao bora na wa kasi zaidi wa mtandao wa Broadband kutoka Smile. Na tunataka kuwashukuru wadau wetu wote kwa kuendelea kutuunga mkono wakati wa kuimarisha shughuli zetu na kupanua mtandao wetu. Tupo na tunakaa. tumejitolea kwa watu wetu wa Zanzibar na Tanzania na tunalenga kuendelea kutoa huduma bora zaidi za mtandao wa 4G LTE,” alimalizia kwa kusema Bibi Zuweina Farah, Meneja wa Smile Tanzania.
Smile Communications, ni kampuni ya Mawasiliano ya Africa yenye shughuli zake nchini Tanzania, Nigeria, Uganda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,ilitangaza operesheni zake katika nchi zote, pamoja na Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...