Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma
Katika mpango mkakati wa Serikali kuhakikisha makao makuu ya nchi yanahamia Dodoma, Serikali inajenga Wizara zaidi ya 21 na Taasisi zake mbili.
Ameyazungumza hayo Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omar Kipanga akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Wizara hiyo katika mji wa Serikaki Mtumba Dodoma.
Waziri kipanga amesema jengo hilo likikamilika litakuwa imegharimu bilioni 15 na fedha hizo tayari Rais Samia ameshazitoa kwa ajili ya mradi huo.
" Mradi huu unaendeleaje vizuri pamoja na kuwa kuna changamoto mbalimbali, kulikuwa na ucheleweshwaji wa siku 20 na tumekaa na kuzungumza na mkandarasi na tumemuagiza kuhakikisha kuwa siku hizo zote zinafidiwa" - Amesema Kipanga.
Aidha Kipanga amesema Wizara ya Elimu itasimamia ujenzi huo kwa kushirikiana na washauri waandamizi kutoka Chuo kikuu Ardhi kupitia kampuni yake tanzu ya ARU built Environment Consulting Company Limited (ABECC) wakishirikiana na washirika kutoka CPI International Limited na ML Engineering Consultancy Company Limited. Na ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika kabla au ifikapo muda wa miaka miwili iliyopangwa.
Kwa upande wake mshauri wa mradi Saudieni Anania amesema mradi huo umefikia wastani wa asilimia tano na mkandarasi ameshalipwa kiasi cha shilingi Bilioni 2.3 sawa na wastani wa asilimia 15 ya gharama za mradi
Hata hivyo Kipanga amempongeza mkandarasi wa mradi huo kwa kuwa kila alichokihitaji katika kuanza kwa ujenzi huo ameviona vipo kamili
Wakati huo huo Naibu Waziri kipanga amempongeza Rais Samia kwa kuhakikisha kuwa Wizara za Serikali zinajengwa Makao makuu Dodoma nae hivyo kutekekeza maono ya muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli ambaye aliaema ni lazima Makao makuu yahamie Dodoma.
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akisikiliza taarifa ya mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma ikisomwa na Mkadiliaji majenzi kutoka chuo cha Ardhi Bw.Saudeni Anania,wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma iliyosomwa na Mkadiliaji majenzi kutoka chuo cha Ardhi Bw.Saudeni Anania,wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akikagua mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Mafundi ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma wakiendelea na ujenzi huo.
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...