Mwandishi Maalum

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt.Eliezer Feleshi amesema kuna haja na umuhimu wa kuwa na vituo vya kutoa huduma ya pamoja ( One Stop Center) kwa wahanga wa visa ya ubakaji na uyanyasaji wa kingono.

Ametoa ushauri huo mwishoni mwa wiki jijini Dar Es Salaam, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi. Lulu Ng’wanakilala ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ijulikanayo kama Legal Service Facility

Amesema uwepo wa vituo hivyo si tu kutaongeza kasi ya kushugulikia visa hivyo lakini pia utaharakisha upatikanaji wa haki kwa wakati na kutoa ahueni kwa wahanga wa matukio hayo.

Na kwa sababu hiyo ameishauri Taasisi ya Legal Service Facility ambayo ni mdau muhumu kulifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na wadau wengine nje ya Serikali kwa kile alichosema kwa sababu wao tayari wanazo pragramu kadhaa wanazoshirikiana na Serikali.

AG Feleshi ametolea mfano wa Nchi ya Afrika ya Kusini ambayo imeazisha vituo kama hivyo vinavyojulikama kama Thuthuzela Care Center na kwamba uwepo wa vituo hivyo na ambavyo vimesambaa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo umerahisisha sana ushughulikiaji wa makosa hayo na utoaji wa haki kwa wakati.

Akifafanua zaidi kuhusu vituo hivyo , Mwanasherika Mkuu wa Serikali , amesema vitu hivyo vitatakiwa kuwa na watoa huduma wenye utaalamu na weledi wa kushughulikia visa hivyo.

“Vituo hivi vinatakiwa kuwa na daktari, polisi, mpelelezi, mwendesha mashtaka, afisa ustawi wa jamii, wataalamu wa saikolojia na ushauri nasaha pamoja na wadau wengine. Inatakiwa mhanga aliye nyanyaswa kingono au kubakwa anapofika kituo hapo anapata huduma zote hapo hapo, kama daktari anakuwapo, kama mpelelezi yupo, kama mwendesha mashataka anakuwapo na polisi anakuwapo”. Anabainisha Mwanasheria Mkuu.

AG Feleshi amebainisha kwamba, kwa uzoefu wake akiwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali lakini pia kama Jaji amekuwa akishughulika kesi za ubakaji na unyanyasi ameshuhudia mashauri mengi kutofikia tamati kutoka na sababu nyingi zikiwamo za upepelezi na ushahidi kuvurugwa.

“Wakati mwingine unaona kabisa hapa kuna kesi ya kujibu na haki inatakiwa kutendeka lakini mara unakuta mpelelezi anashindwa kuifanya kazi yake ipasavyo au ndugu wa mhanga wanaingilia kati kwa kutaka wayamalize kifamilia , kimilia au kwa kuficha ushahidi na hata kumrubuni mhanga”.

Jambo jingine analosema linachangia kutopatikana kwa ushahidi wa kumtia mtuhumiwa hatiani ni kwa wahanga kutokwenda polisi mapema mara baada ya tukio au wanakwenda polisi wakati ushahidi umeshavurugwa.

“Sheria inataka mhanga anapofanyiwa uovu huo aende mara moja kituo cha polisi au kituo cha matibabu, lakini hali ilivyo ama wahanga wengi wanaficha uovu huo kwa sababu mbalimbali au wanakwenda kutoa taarifa wakati ushahidi umeshavurugwa.Nipende kusisitiza kwamba, kuficha kosa ni kosa kisheria” amesisitiza.

Anasema matukio ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono ni very technical katika kuyashughulikia kutoka na mazingira na unyeti wa matuko yenyewe na ndiyo maana uwepo wa vituo hivi utasaidia sana kwa sababu wataalamu wote watakuwa mahali pamoja.

Amesema pamoja na uwepo wa madawati ya jinsia katika vituo vya polisi na uwepo wa mashirikia yasiyo ya kiserikali yanoshughulia visa hivyo bado jitihada zaidi zinahitajika.

Akasema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka tayari yana Divisheni zinazoshughulika na masuala ya Uratibu hivyo Ofisi hizo mbili zitakuwa tayari kutoa ushirikiano katika jambo hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo wa LSF amemshukukuru Mwanasheria Mkuu kwa wazo hilo na kwamba watalifanyia kazi.

Aidha akasema LSF itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika utoaji wa msaada wa kisheria pamoja na kuwaelimisha na kuwawezesha wadau wao na hususani wanawake kuhusu masuala yahusuyo sheria pamoja na kutambua haki zao.Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility Bi. Lulu Ng'wanakilala mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. Bi. Ng'wanakilala alimtembelea AG Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...