Kamati ya Viwanda Biashara na Mazingira imetembelea katika viwanda vya kuzalisha chanjo za mifugo nchini ( HESTER Biosciences Africa Ltd ) na kiwanda cha kuunganisha magari (GFA Vehicle Assemblers) .

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza magari cha GFA Vehicle Assemblers, Ezra Mereng' ameomba Serikali kurekebisha sheria na kupunguza ushuru ili kuwalinda wawekezaji wazalendo kuweza kushindana na wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi,Pia aliishauri serikali kuwaomba waagizaji wa magari (trucks) kuagiza vipuri na kazi ya uunganishwaji ifanyike hapa nichin kuweza kuokoa fedha za kigeni ambazo zingetumika kwa kuagiza magari na badala yake kutanua soko la ajira kwa vujana wetu walioko katika viwanda vya ndani

Kiwand hicho ambacho kipo katika awamu ya pili ya uzalishaji mpaka sasa kimetengeneza magari 420 kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji ambapo kazi nyingi katika kiwanda hicho hufanywa na watanzania waliopata ujuzi kutoka kwa wataalamu wa Kigeni Kwani kiwanda hicho kina wafanyakazi zaid ya mia moja na kati yao 95 ni watanzania na 5 ni wageni kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Akijibu baadhi ya hoja zilizotolwea na wawekezaji hao Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Ashatu Kijaji aliwatoa hofu wawekezaji hao na kuwaambia kwamba serikali ya amwamu ya sita ipo karibu nao na suala la ukatikaji wa umeme ambalo ni miongoni mwa changamoto zilizowasilishwa, Kijaji alisema serikali ipokatika hatua za kuongeza vyanzo vya umeme mkubwa ikiwemo mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere litakuwa mkombozi wa tatizo hilo.

Nae Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Erick Shigongo alisema swala la kubadilisha sheria kumlinda mwekezaji wa ndani (local content) kamati itafikisha bungeni kwani wao ndio wenye mamlaka ya kutunga sharia hizo ili wawekezaji waweze kushindana katika soko na wawekezaji wakubwa kutoka nje .

Kamati hiyo ilitembelea viwanda vya kuzalisha chanjo za mifugo nchini ( HESTER Biosciences Africa Ltd ) na kiwanda cha kuunganisha magari ( GFA Vehicle Assemblers )

Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza magari cha GFA Vehicle Assemblers, Ezra Mereng' akizungumza na
Kamati ya Viwanda Biashara na Mazingira
Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji, Ashatu Kijaji akimsikiliza mtaalamu wa ufundi Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari cha GFA Vehicle Assemblers, Hamadi Ramadhani wakati kamati ya Bunge ya viwanda Biashara na Mazingira walipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha mkoani Pwani jana.

Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza magari cha GFA Vehicle Assemblers, Ezra Mereng' akizungumza na kamati

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Ashatu Kijaji akiangalia magari wakati kamati ya viwanda, biashara na Mazingira ilipofanya ziara katika kiwanda cha magari cha GFA Vehicle Assemblers Kibaha mkoana Pwani

Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji, Ashatu Kijaji akimsikiliza mtaalamu wa ufundi Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari cha GFA Vehicle Assemblers, Hamadi Ramadhani wakati kamati ya Bunge ya viwanda Biashara na Mazingira walipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha mkoani Pwani jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...