Sehemu ya  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika Shirika la Taifa la Madini (STAMICO),jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dustan  Kitandula akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Shirika la Taifa la Madinini (STAMICO) jijini Dar es Salaam.


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wametembelea  na kukagua kiwanda cha kuzalisha mkaa mbadala wa makaa ya mawe  (Rafiki Briquettes)  kilichopo Msasani, jijini Dar es salaam.

Kamati hiyo ilitembelea kiwanda hicho siku tarehe 14 Machi 2022 na kupokelewa na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Madini  na Shirika la Madini la Taifa wakiongozwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa,  Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo.

Akiongea mara baada ya kutembelea kiwanda na kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi Mwenyekiti  wa Kamati  hiyo Mhe. Dustan Kitandula ameipongeza STAMICO kwa kuwa na ubunifu ambao unalenga kuchangia katika jitihada za kutunza mazingira, kuongeza ajira na kuongeza nishati ya kupikia.

Amesema ubunifu  wa STAMICO ni mkubwa na unahitaji pongezi kwa kuwa unakuja kuchangia  katika ongezeko la nishati  kidigitali nchini.

Amesema STAMICO  inatakiwa kuongeza  kasi na kukamilisha taratibu za uzalishaji ili iweze kuipeleka bidhaa hii sokoni kwa kuwa ina uhutaji mkubwa sana sokoni

Aidha ameitaka STAMICO kutanua wigo wa soko kwa kufanya  kampeni ya kutosha ili watumiaji waweze  kupata taarifa  zaidi kuhusu  mkaa huu, sambamba  na kuainisha changamoto  zinazorudisha nyuma kasi ya uzalishaji  ili kuweza kutatua changamoto  hizo kwa pamoja.

Naye Naibu Waziri wa Madini Dkt.Kiruswa ameishukuru Kamati kwa kutembelea mradi huo muhimu na kushukuru kwa ushauri na maelekezo yaliyotolewa yakilenga kuujenga mradi huo ili uwe imara zaidi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse alipata fursa ya kutoa taarifa ya mradi pamoja na faida zake zikiwemo kuongeza mapato  ya Shirika, kuokoa misitu, kuchangia kodi,  kutoa ajira na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha, amekiri kuyatekeleza maoni na maelekezo yote yaliyotolewa na Waheshiwa Wabunge.

Viongozi wengine walioshiriki kwenye ziara hii ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Madini na STAMICO, Mameneja na wataalamu kutoka STAMICO ambao ndio wasimamizi mradi huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Madini  (STAMICO) Dk.Venance Mwase akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini Stella Manyanya wakati kamati hiyo ilitembelea STAMICO.
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini wakiwa STAMICO.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...