Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MKAZI Mwananyamala Ujiji, jijini Dar es Salaam, Bahati Sebugire (36) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka moja la kumlawiti mtoto wa miaka tisa.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Easter Michael mbele ya Hakimu Mkazi, Aaron Lyamuya imedai, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo, Julai 6, 2021 katika eneo la Mwananyama Ujiji, wilayani Kinondoni.
Inadaiwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa alimlawiti mtoto wa kike mwenye Umri wa miaka tisa (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za haja kubwa.
Kwa mujibu upande wa mashtaka pande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na hivyo wameiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Hii ni mara ya pili kwa mshtakiwa Sebugire kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo la kulawiti, kwani mwaka jana alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka hilo katika kesi ya Jinai namba 275/2021.
Hata hivyo kesi hiyo ilifutwa Jumatatu Machi 21, 2022 na mshtakiwa kupelekwa Kituo Cha Polisi Oysterbay na jana mshtakiwa huyo amefikishwa Mahakama hapo na kusomewa upya shtaka moja la kulawiti katika kesi ya jinai namba 84/2022.
Kesi hiyo ilifutwa na mahakama hiyo, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kupeleka mashahidi mahakamni hapo kwa zaidi ya miezi mitatu.
Hata hivyo mshtakiwa huyo ameileza mahakama kuwa, alishasomewa hoja za awali Desemba 2021 hivyo aliomba kesi hiyo ianze kusikilizwa, ombi ambalo Hakimu alilikataa na kumueleza kuwa lazima asomewe hoja za awali kwanza ndipo kesi hiyo ianze kusikilizwa.
Hakimu Lyamuya baada ya kutoa maelezo hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 30, mwaka huu, mshtakiwa amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...