Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 2 Machi 2022 akiwa Jijini Nairobi ameshiriki ibada ya Jumatano ya majivu katika kanisa la Mtakatifu Paulo mtaa wa chuo kikuu cha Nairobi.

Akiongoza Ibada hiyo Paroko msadizi wa Kanisa katoliki la Mtakatifu Paulo Padri Edwin Hunja amewataka waumini kutumia kipindi hiki cha kwaresma katika kutafuta msamaha na huruma ya mwenyezi Mungu pamoja na kujielekeza kutenda matendo yaliyo mema. Padri Paulo amesema mwezi huu wa Kwaresma unapaswa kutumika katika kuwapatanisha wale wanaofarakana na kombea dunia kuwa sehemu ya Amani.

Ibada ya majivu kwa waumini wa Imani ya kikristo ni mwanzo wa mfungo na kipindi cha kwaresma kuelekea sikukuu ya pasaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...