Kamati ya Bunge ya Ukimwi,
Kifua Kikuu, Madawa ya Kulevya na Magonjwa Yasiyoambukiza wakiwa kwenye picha ya pamoja |
NA MWANDISHI WETU, GEITA.
MJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi, Kifua Kikuu, Madawa ya Kulevya na Magonjwa Yasiyoambukiza Neema Lugangira ametaka maji taka yenye zebaki yasiingie kwenye ziwa Victoria kutokana na kuwa na athari kwa binadamu.
Mbunge Lugangira aliyasema hayo wakati wa kamati hiyo ilipotembelea Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) na hilo linatokana na kudaiwa Maji Taka kutoka Migodini inaingia Ziwa Victoria na ina Kemikali ya Zebaki nyingi hatua ambayo ndio kiini cha ongezeko kubwa sana la magonjwa ya Kansa kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo na Kagera anapotokea mbunge huyo
Akijibu hoja hiyo Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Molel alikiri ni kweli ukienda Hospitali ya Ocean Road wagonjwa wengi wa Kansa wanatoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa hivyo aliahidi kuwa Wizara ya Afya kufanya Utafiti kujua nini kinasabisha tatizo la Magonwa ya Kansa kukua kwa kasi kubwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Mhe Dkt.Steven Kiruswa aliichukua changamoto hiyo na kuhaidi kwamba Serikali inachukulia jambo hili kwa uzito mkubwa na tayari imeshaweka mikakati kambambe ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2029 Serikali itakuwa imekomesha kabisa matumizi ya Kemikali ya Zebaki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...