………………………………

Na John Walter -Manyara

Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ametoa agizo kwa Viongozi wa wilaya,tarafa, Halmashauri,wakuu wa Taasisi, kata na vijiji katika mkoa huo kuhakikisha wanapanda miti na kutunza mazingira katika maeneo yao yanayowazunguka.

Aidha Makongoro ameagiza zoezi hilo lifanyike katika kila kaya,shule za msingi na sekondari,kwenye maeneo ya taasisi za kidini,maeneo yanayomilikiwa na taasisi binafsi,maeneo ya kibiashara,viwanja vya Michezo na kwenye viwanda.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,kubadili tabia na kuboresha Usafi wa Mazingira iliyofanyika kijiji Cha Riroda wilayani Babati, Makongoro amesema zoezi la kutunza mazingira kwa ajili ya maendeleo ni lazima liwe shirikikishi na si kuiachia serikali peke yake hivyo jitihada zinahitakika kutoka serikali kuu,serikali za mitaa,taasisi za serikali na zisizo za serikali,sekta binafsi na wadau wengine katika jamii.

Alisema kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali za kimazingira ambapo alitaja baadhi ya changamoto hizo ni uharibifu wa Ardhi ,uharibu wa misitu,uharibifu wa vyanzo vya maji,uharibifu wa makazi ya viumbe wa majini pamoja na upotevu wa bioanuai.

Hata hivyo amewasisitiza wananchi kuendelea kutunza mazingira pamoja na kuhakikisha wanaotesha miti ya asili ili kupunguza ukame unaoweza kusababishwa na upotevu wa maji ardhini.

Alisema Kuhifadhi mazingira sio jukumu la serikali peke yake bali ni la kila mtu kwa nafasi yake kwa faida ya afya zetu na viumbe wengine na kwa kizazi Cha Sasa na kijacho.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo amesema ni muhimu kila mmoja akatimiza wajibu wake katika kutunza mazingira ili kuepuka athari mbalimbali zinazotokana na uharibifu wa mazingira ikiwemo ukosefu wa mvua.

“Kama mtu utashindwa kutunza mazingira,unakuwa umejinyima haki mwenyewe” alisema

Kwa upande wa Makamu mkurugenzi wa WaterAid Tanzania Humphrey Mwiyombela ambao ni wadau wa Mazingira,amesema wataendelea Kushirikiana na serikali utunzaji wa Mazingira ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi.
Kauli mbiu inayoongoza kampeni hiyo inasema “Mazingira yako,uhai wako,yatunze daima”


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...