Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Atupele Mwakibete, amelitaka Baraza la Wafanyakazi la Sekta hiyo kutafuta suluhu ya changamoto za wafanyakazi na kuweka usawa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Mwakibete amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa baraza la Wafanyakazi lililowakutanisha kwa ajili ya kujadili masuala ya wafanyakazi na kupitia mpango wa Bajeti kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.

“Hakikisheni mnashughulikia malalamiko ya watumishi sehemu mnazozisimamia ili kuweka usawa na utendaji kazi mzuri kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kupewa nafasi za kujiendeleza kielimu”, amesema Mwakibete.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migire, amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa kwa sasa Sekta inafanya uhakiki na uchambuzi wa madeni ya watumishi hususan wastaafu na kuweka mikakati thabiti ya kulipa madeni hayo.

“Baraza hili linakutana hapa kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa mpango na Bajeti ya Sekta ya Uchukuzi kwa mwaka 2020/2021 ikiwa ni pamoja na masuala mbalimbali yanayowahusu watumishi ”, amefafanua Migire.

Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Uchukuzi limeshirikisha Wajumbe wa Baraza ambao ni wakuu wa Idara na Vitengo, wakuu wa taasisi zote zilizoko chini ya Sekta hiyo pamoja na viongozi wa chama cha wafanyakazi.

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Atupele Mwakibete, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Uchukuzi (hawapo pichani), wakati akifungua baraza hilo katika ukumbi wa Mabele, Jijini Dodoma


Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Uchukuzi), Bw Gabriel Migire akisisitiza Jambo kwa Baadhi ya wajumbe wa baraza la Wafanyakazi Sekta ya uchukuzi (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa baraza hilo lilifanyika katika ukumbi wa Mabele, Jijini Dodoma.


Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara hiyo anayesimamia Sekta ya Uchukuzi, Atupele Mwakibete (hayupo pichani) wakati wa akifungua baraza hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mabele, Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...