Na Mwandishi Wetu
Katika Kipindi cha mwaka mmoja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kumekuwa na mafanikio ya kiongozi wa kusimamia utendaji na kufanikiwa kuvutia wawekezaji kwa wingi nchini ikiwemo sekta ya madini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya kuchambua kurasa za siku 365 za Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kongamano iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Waziri ameipongeza STAMICO kwa kuwa na mafanikio yanayooneka kwa kipindi kifupi sana na kuitaka kuendeleza mafanikio hayo yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya Sita ikiwani sehemu ya kuendeleza mazuri yote yaliyoachwa na uongozi wa awamu tano zilizopita na amerekebisha maeneo yenye makosa kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuondoa utegemezi.
Akizungumzia Mafanikio ya Shirika Bw. Deusdedith Magala kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Vanance Mwasse amesema, katika mwaka mmoja au siku 365 za Mama, STAMICO imefanikiwa kuongeza mapato ya ndani na kwa kuanza kujiendesha kwa faida. Pia ni katika awamu ya sita ambapo kwa mara ya kwanza Shirika limeweza kutoa gawio Serikalini.
Aidha, Bw. Magala ameeleza mafanikio ni pamoja na ujenzi na ufunguzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha madini ya dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery chenye uwezo wa kusafisha kilo 480 za dhahabu kwa siku kwa kiwango cha kimataifa cha asilimia 99.99.
Aidha Bw. Magala amesema Shirika limeweza kununua mitambo ya kisasa nane (8) ya uchorongaji yenye thamani ya Bilioni 11.2 na vilevile tumeweza kupata kandarasi za uchorongaji zenye jumla ya shilingi bilioni 33 katika migodi mikubwa kama GGM, Buckreef na Buhemba ukilinganisha kandarasi zenye thamani ya Shilingi bilioni 17 za mwaka uliopita.
Bw. Magala ameainisha mafanikio mengine yakiwemo kuanzisha mradi wa kutengeza mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe (Coal Briquttes). Kuboresha vituo vya mfano vya wachimbaji wadogo na kuwaunganisha na taasisi za kibenki ili waweze kukopesheka pamoja na maboresho makubwa yaliyofanyika kwenye Vituo vya Mfano vya Lwamgasa, Katente na Itumbi.
Pia Shirika limesaini mikataba na benki za CRDB, NMB na KCB ili kuanza kuwakopesha wachimbaji wadogo walikuwa hawaaminiwi kukopeshwa. Pia Shirika limesaini makubaliano na GST ili kushirikiana kuainisha maeneo yanayofaa kwa kuwapa wachimbaji wadogo. Sambamba na hilo, Shirika linaagiza mashine tano za Uchorongaji kwa ajili ya kuwasaidia wachimbaji wadogo.
Hafla hiyo iliyobebwa na kauli mbiu isemayo " Mama yuko Kazini", imewakutanisha wadau kutoka Wizara na taasisi mbalimbali ambazo zilipata fursa ya kueleza jinsi zilivyofanikiwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...