Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akimkabidhi vifaa tiba Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, Dkt. Msafiri Marijani kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika hospitali hiyo. NSSF imefanya makabidhiano hayo wakati wa kuelekea kilele cha siku ya Wanawake Duniani Machi 8

Katika kuelekea kilele cha siku ya Wanawake Duniani Machi 8, baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  kukabidhi msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar. NSSF kupitia sera ya kuchangia na kudhamini imekuwa ikiwajibika katika jamii (CSR) kwa kutoa misaada katika sekta ya afya, elimu , michezo na jamii kwa ujumla.



 Na MWANDISHI WETU

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar ambavyo ni vitanda vya kujifungulia pamoja na mashine za kupimia shinikizo la damu ambavyo vitasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanaopata huduma katika hospitali hiyo.

Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele alisema Mfuko unatambua mahitaji ya jamii kwa kutoa misaada mbalimbali kupitia Sera ya Mfuko ya Uchangiaji na Udhamini (CSR), moja ya eneo ambalo wanatoa misaada ni kwenye sekta ya afya na hivyo wafanyakazi wanawake wameguswa ndio maana Mfuko umetoa msaada huo ili kutatua changamoto za upungufu wa vifaa tiba katika hospitali hiyo.

“NSSF katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8 na mwaka huu ikiwa na kauli mbiu isemayo ‘Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu’ Mfuko umeamua kusaidia vifaa tiba katika hospitali hii ya Mnazi Mmoja ili kuokoa maisha ya ndugu zetu wanaopata huduma,” alisema Lulu.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt. Msafiri Marijani alisema kwa niaba ya uongozi wa hospitali hiyo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya Zanzibar, wanaishukuru NSSF kwa kutoa vifaa tiba hivyo ambavyo vimetolewa kipindi ambacho hospitali hiyo ina uhitaji wa vifaa tiba mbalimbali na kuahidi vifaa hivyo kutumika kwa lengo lililokusudiwa.

Mwenyekiti wa Wanawake NSSF, Vaileth Segeja, alisema wametoa msaada huo kwa sababu Mfuko una sera ya kutoa misaada katika jamii, na kutoa wito kwa wanawake wote waliopo katika sekta isiyo rasmi kujiunga na Mifuko ya hifadhi ya jamii ukiwemo wa NSSF na ZSSF kwa ajili ya maisha yao ya sasa na baadaye.

Kwa upande wake, Nassor Hassan ambaye ni Afisa Utawala wa ZSSF alisema kazi kubwa ya Mifuko ya hifadhi ya jamii ni kuihifadhi jamii pale inapopata janga ikiwemo ugonjwa na ndio maana NSSF iliamua kutoa msaada wa vifaa tiba hivyo ili vikasaidie kuokoa maisha ya wananchi.






















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...