Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema mwongozo wa program ya michezo na sanaa ya mtaa kwa mtaa imekamilika na utawasilishwa kwenye kikao kazi cha maafisa utamaduni na michezo kinakachofanyika mwanzoni mwa mwezi Aprili 2022 jijini Dodoma.

Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Machi 26,2022 mara baada ya ziara yake ya kikazi aliyoambatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Hassan Abbasi kukagua miundombinu mbalimbali ya uwanja wa Benjamini Mkapa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa chumba maalum cha mazoezi ya viongo (Gym) baada ya kupata wasilisho kuhusu program mtaa kwa mtaa kutoka Idara ya Maendeleo ya Michezo na Baraza la Michezo (BMT) nchini.

Mhe. Mchengerwa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeamua kuratibu na kuendesha mashindano ya michezo ya kitaifa yatakayojumuisha michezo mbalimbali ambayo yataanzia katika ngazi ya mtaa na kujulikana kwa jina la SAMIA CUP -Mtaa kwa Mtaa kisha kwenda kitaifa ambapo yataitwa SAMIA TAIFA CUP.

Mhe Mchengerwa ameongeza” katika michezo”mtaa” umepewa maana mbalimbali ili viongozi wa Serikali waweze kusimamia, kutembelea na kuweka mageuzi stahiki kwa maendeleo ya Sanaa nzima”

Akitoa wasilisho hilo Mkurugezni wa Michezo nchini Yusufu Singo amefafanua dhana ya mtaa kwa mtaa katika maana tatu ambapo amesema maana ya kwanza ni mtaa ikiwa na maana ya mtaa wa sasa wa Serikali ambapo amesema hadi sasa mitaa inafika takribani 400 nchi nzima.

Aidha, Singo amesema maana ya pili ya mtaa inajumuisha shule, vyuo na taasisi ambapo amesema hii itajumuisha mashindano kama ndondo CUP, mashindano ya vijana ya TFF, Coca Cola, Umitashumta, umiseta na mashindano ya taasisi kama SHIMIWI,SHIMUTA NA SHIMISEVITA.Amesema maana ya mwisho ya mtaa ni ligi mbalimbali za kitaifa za michezo.

Mhe. Mchengerwa ameeleza malengo ya program hii kuwa ni pamoja na kuibua vipaji vya michezo na Sanaa katika ngazi ya mitaa, vijiji, kata, tarafa, Wilaya na Mikoa na hatimaye Taifa,kuunganisha na kujenga mshikamano katika jamii pamoja na ujenzi wa uchumi binafsi na nchi kwa ujumla pamoja na kutoa fursa kwa wananchi kwa ngazi zote za Serikali kushiriki kwa vitendo shughuli za Michezo na Sanaa ili kunufaika na faida zake.

Amesisitiza kuwa mkakati wa michezo mtaa kwa mtaa ni mpango mpya uliobuniwa na Wizara ili kuhakikisha kuwa wananchi hususan vijana wanapatiwa fursa kubwa ya kuoonesha vipaji vyao katika ngazi zote.

Ameitaja michezo itakayohusishwa katika program hii kuwa ni pamoja na riadha, mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mchezo wa netiboli, mpira wa wavu, michezo ya jadi na sanaa za ndani.

Amesema matokeo tarajiwa katika program hii ni vijana zaidi ya 80,000 kuweza kushiriki katika ngazi ya kata hadi mkoa, vijana kutoka ngazi za vijiji na mtaa kuweza kupata nafasi ya kuonekana kwenye ngazi ya taifa na vijana wenye vipaji kupata nafasi ya kujiunga na maalum za michezo (academies).




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...