· Ni katika jitihada za kujiimarisha kuwa chaguo pekee la mshirika wa huduma za kidijitali kwa wafanyabiashara nchini Tanzania

 RAHA Liquid Telecom sasa kutambulika rasmi kama - Liquid Intelligent Technologies, ikiwa ni sehemu ya kampuni ya Cassava Technologies. Utambulisho huu mpya ni sehemu ya mabadiliko mapana ya kibiashara kutoka kutoa huduma za kimawasiliano na kuwa kampuni inayotoa huduma za kiteknolojia kiukamilifu kwa wafanyabiashara wa nyumbani.

Kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita, Liquid imejiimarisha kwa uthabiti kama kampuni ya Kiafrika inayoongoza kwa huduma za miundombinu ya kidijitali ikiwa na mtandao mpana unaozunguka zaidi ya kilometa 100,000. Kubadilika kwa RAHA Liquid Telecom na kuwa Liquid Intelligent Technologies kunaonyesha kujizatiti kwa kampuni katika kubadili bara la Afrika kwenda kidijitali kupitia huduma za kibiashara za mtandao, usalama dhidi ya wizi wa kimtandao zikiwa ni sehemu ya huduma zake za kimawasiliano pamoja na uwezo wa uunganishaji.

Denny Marandure, Afisa Mtendaji Mkuu wa Liquid Intelligent Technologies Tanzania, amesema kuwa: “Mageuzi haya ya kampuni ya RAHA Liquid Telecom kuwa Liquid Intelligent Technologies yamefungua fursa lukuki na ni hatua ya kusonga mbele kuelekea kwenye kuwa na uchumi unaoendeshwa kidijitali. 

Siku zote Liquid imekuwa ikiamini kuwa ushirika baina ya taasisi binafsi na za umma ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi, na kampuni yetu imefanikiwa kushirikiana na serikali mbalimbali barani Afrika. Tunatarajia kushirikiana na serikali kuisaidia kuyafakia kwa ukamilifu malengo iliyojiwekea ambayo ni msingi wa mafanikio ya muda mrefu ya Tanzania.”

Kama mshirika wa Microsoft Gold, Liquid Intelligent Technologies tunazipambanua upya huduma za kiuunganishaji, kimtandao, na usalama mtandaoni kupitia ushirika wetu wa kimkakati na makampuni yanayoongoza duniani, kuleta ubunifu kwenye ufanyaji wa biashara, huduma za kisasa za kimtandao, na usalama wa hali ya juu barani Afrika.

Tukiwa tunaelekea kwenye mfumo imara wa kiusalama kutokana na huduma za kimtandao, hivi karibuni Liquid Intelligent Technologies imezindua kitengo chake cha biashara kinachojihusisha na Usalama wa Mtandaoni, ambacho kwa kipekee kimejizatiti katika utoaji wa suluhisho la usalama, kulinda taarifa za kibiashara kwenye mfumo mzima wa ufanyaji shughuli zako.

Akizungumzia kuhusu mabadiliko hayo, Adil Youssefi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Liquid Intelligent Technologies wa Masoko ya Ukanda wa Afrika ya Mashariki, amesema kuwa, “Mabadiliko haya ni katika kuwahakikishia wateja wetu wote wa nchini Tanzania kuwa sisi ni watoaji wa huduma zote za kiteknolojia ambapo tunazileta kwa pamoja huduma za mtandaoni kwa mfumo wa kompyuta, usimamizi wa huduma, na suluhisho la usalama wa kimtandaoni. 

Tumewaletea huduma za thabiti na za kisasa barani kote, na tunaamini kwamba uwepo wetu nchini Tanzania utahakikisha uunganishwaji wa uhakika wakidijitali kwa Watanzania wote.”
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Liquid Intelligent Technologies Tanzania,Denny Marandure,akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar Es Salaam kuhusu  Utambulisho mpya wa iliyokuwa kampuni ya  RAHA Liquid Telecom na sasa kuwa Liquid Intelligent Technologies.

Marandure amesema Mageuzi haya ya kampuni ya RAHA Liquid Telecom kuwa Liquid Intelligent Technologies yamefungua fursa lukuki na ni hatua ya kusonga mbele kuelekea kwenye kuwa na uchumi unaoendeshwa kidijitali. 


 Afisa Mtendaji Mkuu wa Liquid Intelligent Technologies Tanzania,Denny Marandure akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar Es Salaam wakati wa Utambulisho mpya wa iliyokuwa kampuni ya  RAHA Liquid Telecom na sasa kuwa Liquid Intelligent Technologies.


Mkutano ukiendelea na Waandishi wa Habari
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Liquid Intelligent Technologies Tanzania,Denny Marandure akieleza kwa Waandishi wa Habari namna iliyokuwa kampuni ya  RAHA Liquid Telecom na sasa kuwa Liquid Intelligent Technologies ilivyosambaa maeneo mbalimbali Barani Afrika huku ikiwahudumia mamilioni ya wateja wao.


Mtaalamu wa masuala ya TEHAMA kampuni ya  Liquid Intelligent Technologies Evans Lwanga akieleza Mabadiliko ya Kampuni hiyo kuwa ni katika kuwahakikishia wateja wao wote wa nchini Tanzania wanapata huduma zote za kiteknolojia, ambapo amesema kwa pamoja wanazileta huduma za mtandaoni kwa mfumo wa kompyuta, usimamizi wa huduma, na suluhisho la usalama wa kimtandaoni. 

Mkuu wa Masoko kampuni ya Liquid Intelligent Technologies, Deo Ngonyani akieleza kuhusu namna kampuni hiyo itakavyoweza kuwahudumia wateja wa kila aina na popote pale walipo kwa uhakika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...