Na Yeremias Ngerangera,Songea

Waziri wa maliasili na utalii Dokta Damas Ndumbaro ameelezea juhudi za uhifadhi katika maeneo mbalimbali ya mbunga za wanyama kuwa zinatokana na mafanikio aliyafanya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluu hassani katika kuhakikisha sekta ya utalii inahimarishwa zaidi.

Dokta ndumbaro aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini songea ambapo alifafanua kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amekuwa mstari wa mbele kuutangaza utalii kwa lengo la kuongeza idadi kubwa ya watalii wanaokuja toka mataifa mbalimbali kuja kutembelea hifadhi pamoja na mbuga za wanyama zilizopo hapa nchini.

Alisema kuimarika kwa uhifadhi wa maliasili,wanyama poli na misitu kuna mambo 10 yaliowekwa katika kuhakikisha kuwa Tanzania inapata watalii wengi ikiwa ni pamoja na kanuni za jeshi la uhifadhi zimepitishwa na kutambuliwa kuwa jeshi kamili la uhifadhi wa wanyama poli na misitu.

Alisema kupungua kwa ujangili ikiwemo kuuwawa kwa tembo na biashara ya pembe za ndovu kuwa unapungua na kwamba idadi ya faru na simba inaongezeka kutoka mikakati iliowekwa na serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kwa wadau mbalimbali wa uhifadhi.

Dokta ndumbaro ambae pia ni mbunge wa songea mjini alifafanua kuwa kuongezeka kwa idadi ya watalii na mapata,idadi ya watalii wa ndani waliotembelea maeneo ya hifadhi pia iliongezeka kutoka watalii laki 5 na 62 elfu na 549 mwaka 2020 hadi watalii laki 788 elfu 933 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 40.2 .

Alisema kuwa vile vile mapato yatokanayo na utalii wa ndani katika maeneo yaliohifadhiwa yaliongezeka kutoka shilingi billion 9.7 mwaka 2020 hadi shilingi bilioni 12.4 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 27,8 na idadi ya watalii wa nje iliongezeka kwa asilimia 48.6 kutoka watalii laki 620 elfu 827 mwaka 2020 hadi watalii laki 922 elfu 692 mwaka 2021ambapo mapato nayo yaliongezeka kutoka dola za marekeni milioni 714.59 mwaka 2020 hadi million 1,254.4 mwaka 2021 sawa na angezeko la asilimia 76.

Alifafanua zaidi kuwa nchi imetmbuliwa kwa kupatuwa tuzo na heshima mbalimbali katika uhifadhi na utalii hivyo Tanzania kutambuliwa na UNWTO kama nchini inayo stahimili na kufabya vizuri zaidi duniani katika utalii wakata wa janga la uvico 19 kwa mwaka 2020 na 2021 Tripadvisor kupitia travelers choice destination-Afrika imeziorodhesha Zanzibar na jiji la Arusha kuwa miongoni mwa maeneo 10 bora ya shughuli za utalii barani afrika.

Alisema Tanzania ilichaguliwa na taasisi inayoanda tuzo za utalii duniani word travel award(WTA) kuwa nchi inayoongoza kwa shughuli za utalii barani afrika(Africans leading destination for the year 2021) na tuzo ya utalii wa bara (continent tourlism award 2021)iliotolewa na badi ya utalii ya afrika(African tourlism board) wakati wa onesho la kwanza la EARTE lililofanyika jijini Arusha oktoba 2021.

Waziri wa maliasili na utalii dokta ndumbaro alisema kuwa kutokana na juhudi za mheshimiwa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania samia suluu hassani katika kuleta maendeleo kwa wananchi,Tanzania iliweza kupata mkopo wa fedha maarufu ka,a fedha za uvico 19 kwa upande wa wizara ya malisili na utalii gfedha hizo zimewezesha kukarabati miundombinu ya utalii ikiwemo barabara na madaraja katika maeneo ya hifadhi.

Aliongeza kuwa kumekuwa na jitihada mahsusi za mheshimiwa Rais samia katika kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia program maalum za royal tour kupitia program huo mtandao maarufu wa habari nchini marekani wa the grio umetambua juhudi za rais samia kaika kuingoza vyema sekta ya utalii nchini na kuifanya Tanzania kuwa kivutio cha kwanza cha utalii afrika mwaka 2022 na imesababisha kuongezeka watalii wa wawekezaji mbalimbali ikiwemo utali na kuongezeka kwa juhudi za kutangaza utalli kwa kuvutia wawekezaji zaidi pamoja na kuwepo mpango wa kutumia ndege za kampuni ya emirates kutangaza vivutio vya utalii.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...