Na Khadija Kalili , Kibaha
Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Tumbo leo jana Machi 5 amewaogoza wanawake na kuwatembelea wafungwa na mahabusu walioko katika Gereza la Mkuza lililopo eneo la Picha Ndege Kibaha na kuzungumza na wafungwa hao akiwa ameambatana na Viongozi wa Gereza Hilo.
Mara baada ya kuwasililiza wafungwa hao ambao alisema kuwa wamempa salamu zao kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa wanashukuru kwamba wanaishi vizuri ndani ya Gereza hilo huku ikielezwa kuwa changamoto kubwa walitokuwa nayo ni ukosefu wa uzio.
Akizungumza mara baada ya kuwaona wafungwa hao RAS Mwanasha alisema kwamba atazidikisga salamu zao kwa Mheshimiwa Rais Mama Samia ,huku akiahidi kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itatoa.mifuko 100 ya sauji ikiwa ni katika kuchangia ujenzi wa uzio wa Gereza Hilo ambalo hivi sasa halina uzio.
Aidha katika ziara hiyo ambayo RAS aliwaongoza jopo la wanawake kutoka Mkoa wa Pwani waliofika gerezani hapo walupeleka misaada mbalimbali ikiwemo, Chakula, mafuta ya kupaka, sabunj za kuongea na kufulia, mafuta ya kupaka na 'sanitizer', taulo za kike na taulo za watoto vilivyotolewa na kina mama wa Mkoa wa Pwani pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Sara Msafiri.
"Pamoja na kumshukuru Mwenyeezi Mungu pia tuunashukuru. Uongozi wa Gereza kwa kutupokea ,sisi kama wanawake wa Mkoa wa Pwani lichabya kuwa ni viongozi tumewiwa kujakuwafariji kwa kuwatembelea wafungwa na mahabusu ikiwa ni katika shamrashamra za kuelekea kilele cha wanawake duniani ambayo itaadhimishwa duniani kote ifikapo Machi name"alisema Mhandisi Mwanasha.
Maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani itaadhimishwa kimkoa katika Halmashauri ya Chalinze huku kauli mbiu ya mwaka huu inasema 'Haki na Usawa kwa maendeleo Endelevu'.
Mara baada ya kutoa misaada hiyo pia RAS alipanda mti mmoja aina ya Mtiki ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ikiwa ni katika kuunga juhudi za kutunza mazingira zinazoendelezwa na Makamu Rais Dkt.Philip Mpango.
Mkuu wa Gereza la Mkuza Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP) George Osindi alimshukuru RAS huku akimuomba azifikishe salamu kwa Mkuu wa Mkoa kuwa wanaomba msaada kama huo endelevu na ufanyika katika Magereza zingine za Mkoa ."Tunaomba kama itawezekana tupatiwe msaada kama huu Ili uweze kupeleka katika magereza mengine kwani ndani ya Mkoa tunayo Magereza Saba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...