Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa  amesema wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2021 wanayo nafasi ya  kubadili  machaguo ya  tahasusi (Combination) na kozi mbalimbali wanazohitaji kusoma kulingana na ufaulu wao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 29 Machi, 2022 Jijini Dodoma, Mhe. Bashungwa amesema, hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne kutokujaza fomu (Selfom) kwa uhakika  wakati wanachagua combination zau kozi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo yao.

“Ofisi ya Rais -TAMISEMI imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzi data taarifa zilizo kwenye fomu za mwanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni, hii inazoa nafasi kwa wanafunzi kuweza kufanya mabadiliko ya machaguo yao” amesema Bashungwa

Ameendelea kukufanua kuwa  Serikali imetoa fursa  kwa  wahitimu wa  Kidato cha Nne  kubadili  machaguo yao ili kutoa nafasi zaidi kwa mwanafunzi kusoma tahasusi au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalam  ambao unaendana na machaguo yake  hapo baadae.

“Amewataka  wazazi kushiriki kikamilifu  na  kukubaliana na  mwanafunzi  katika  zoezi hili  ili  pasiwepo na  malalamaiko yoyote ya  mwanafunzi kuwa  amepangiwa machaguo ambayo hakuyachagua hapo baadae” Bashungwa

Ameongeza kuwa zoezi la kubadilisha tahasusi kwa mwanafunzi linafanyika kwa utaratibu wa kuingia kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi (student Selection MIS) kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz kwa kutumia namba ya mtihani.

Ameshuri walezi/wazazi na wanfunzi kuendelea kutumia dawati la huduma  kwa wateja kupitia barua pepe helpdesk@tamisemi.go.tz au  na kituo cha huduma kwa wateja kwa simu namba +255 262 160 20 na +255 735 260 210 au fika katika ofisi za Mamlaka za Serikali za Mitaa.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...