Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri nchini ya Sportpesa imezindua promosheni mpya ya Bet Bonanza kwa lengo la kutoa pesa zaidi kila siku kwa Wateja wake sambamba na wachezaji wengine wa michezo ya kubashiri kupitia mitandao ya Vodacom (M-Pesa) na Artel (Airtel Money).

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni hiyo, Tarimba Abbas amesema amesema Promosheni hiyo imeanza Machi 8, 2022 ambapo washindi wa Promosheni hiyo watazawadiwa Shilingi Elfu Ishirini (Tsh. 20,000/-) kwa kila siku, kwa washindi kumi kutoka Airtel Money na M-Pesa.

Tarimba amesema Promosheni hiyo itadumu kwa siku 35 hadi Aprili 12, 2022, sambamba na zawadi za kila siku pia, kutakuwa na zawadi za kila wiki ambayo ni Shilingi Milioni Moja (Tsh. 1,000,000), amesema mwisho wa Promosheni, mshindi atapata zaidi ya Shilingi Milioni 15 (Tsh. 15,888,000).

Tarimba amesema Promosheni hiyo inatoa fursa kwa wachezaji wa Sportpesa kushiriki vizuri katika ubashiri wa Ligi mbalimbali duniani, na zaidi ya bashiri za kawaida ambazo zina ujazo mwingine.

Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa M-Pesa Kelvin Nyanda amewakaribisha Wateja wa Mtandao wa Vodacom kushiriki kubashiri kwa Bet Bonanza na kujishindia Pesa zaidi kupitia Promosheni hiyo.

Naye, Meneja Biashara wa Airtel, Aggrey Charles amehimiza kushiriki Promosheni hiyo kupitia Menu ya Airtel Money ya *150*60# ili kuweza kushiriki bashiri hizo au kupitia ‘Application’ ya Airtel. Promosheni hiyo ni kwa Watumiaji waliojisajili Sportpesa, Wateja wa Vodacom na Airtel.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni y Sportpesa, Abbas Tarimba (wa pili kutoka kulia) akizungumza wakati wa utambulisho wa Promosheni ya Bet Bonanza ambayo watumiaji wake watashinda zawadi ya pesa kila siku. Wa kwanza kutoka kulia ni Meneja Biashara Airtel, Aggrey Charles, wa Tatu kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa M-Pesa, Kelvin Nyanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...