Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogoro akiwashukuru wadau mbali mbali waliochangia na kujitokeza kwa  kuhamasisha mbio hizo na kutangaza vivutio vya utarihi katika wilaya yake na kuwataka wananchi wote kwa ujumla kumuunga mkono Raisi wetu Mama Samia Hassan kushirikiana naye kwa pamoja lengo ni kuijenga nchi yetu na kutangaza utarihi wetu wa nchi (picha na Ashrack Miraji).
Wadau mbalimbali wakijitokeza kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Same katika mbio za kilometa  5 had 10 lengo likiwa kutangaza utarihi wa wilaya ya same kama mbuga ya wanyama Mkomazi na milima ya shengena yenye vivutio tofauti vinapatika katika wilaya hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Tanapa Taifa  William Mwakilema  (wa pili kulia) akikimbia  mbio za kilometa tano baada ya kuzindua rasmi mbio hizo  kwenye mashindano ya riadhaa, lengo kubwa ni kutangaza vivutio vya utarihi wa ndani katika Wilaya ya Same Mkoa Kilimanjaro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi,  anayefuatia ni  Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogoro sherehe hizo zimefanyika katika mbuga ya Mkomazi na kujionea vivutio mbali mbali vya utarihi katika wilaya ya Same
 


WADAU mbalimbali wameshiriki tamasha la Same Rhino Tourism Fun Run ambalo limeandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Edward Mpogoro kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani uliopo kwenye Wilaya hiyo.

Baadhi ya wadau ambao wameshiriki tamasha hilo ni viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya, Mkuu wa Wilaya Arusha Said Mtanda na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Basilla Mwanukuzi .Mgeni rasmi alikuwa  William Mwakilema ambaye ni Kamishna wa Uhifadhi TANAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...