Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) Bi, Latifa Mohamed Khamis pamoja na Mrajisi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Dr.Benson Ndiege leo tarehe 23 Machi, 2022 katika Ofisi za Tume jijini Dodoma wamesaini makubaliano yenye lengo la kuwawezesha wana ushirika na wakulima kupitia Vyama vya Ushirika nchini kuzalisha bidhaa zao kwa tija ili kufikia masoko endelevu .

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi.Latifa  amebainisha kuwa Progamu hiyo inalenga kuongeza thamani za bidhaa za ndani na kisha  kuwaendeleza wazalishaji na  hatimaye waweze kuwa na   uwezo wa kutumia fursa za biashara na masoko ya ndani na nje ya nchi

Pande zote mbili Kwa pamoja zimeridhia kuwa na mabadiliko ya kasi katika sekta ya biashara ili kwenda sambamba na  Serikali ya awamu ya Sita   inayohimiza uongezwaji wa thamani kwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini ili kuwaletea wananchi maendeleo yenye tija.

Kwa Upande wake Dr.Benson Ndiege Wamevisihi Vyama vya Ushirika nchini kuhakikisha vinashiriki kikamilifu katika programu zilizoainishwa katika makubaliano haya kwa kuunga mkono jitihada za Mhe. rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  kuleta mabadiliko kwenye uchumi wa nchi yetu kuwafikia walengwa .

Makubaliano hayo yanalenga ushirikishwaji katika programu za TanTrade za kukakikisha bidhaa za Vyama vya Ushirika zinapatiwa masoko endelevu ambapo wanachama wa vyama vya ushirika watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo Pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa zao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...