Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
SHIRIKA la uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) ,limeingia makubaliano na Serikali ya Burundi, Congo na Tanzania kwa kufanya ukaguzi wa viwango vya ubora katika Meli zinazo fanya safari za abiria na mizigo kupitia Ziwa Tanganyika lengo ikiwa ni kuhakikisha usalama na utunzaji bora wa ma zingira ziwani.
Akizungumza Mkoani Kigoma jana, mara baada ya kikao cha pamoja na mabalozi na wafanya biashara wa meli hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Usalama, ulinzi na Utunzaji wa Mazingira TASAC, Selestine Mkenda, alisema makubaliano waliokubaliana ni kwamba meli zote za abiria zitatakiwa kuonesha vyeti vinavyo onesha uwezo wa kubeba abiria,viti vyote vya abiria kufungwa kwenye sakafu ya chombo.
Alisema abiria wote wanaoondoka na chombo husika kuacha majina yao na idadi yao katika ofisi ya Tasac, meli zote kuwa na maboya kwa ajili ya usalama pia kuwa na vikingio vya uchafu unaotokana na binadamu lengo ikiwa ni kutunza mazingira na kuzuia uchafuzi wa ziwa Tanganyika.
" katika makubaliano haya yatazingatia vigezo vinavyo simamiwa na mamlaka za usafirishaji majini katika Nchi zote mbili, meli zote zitatakiwa kuja na vyeti vinavyo onyesha uwezo wa chombo husika kutoka mamlaka ya Congo au Burundi na zitafanyiwa ukaguzi na maafisa wa Tasac na majina ya abiria yataandikwa kama kumbukimbu hata wakati wa uokoaji kujua kulikuwa na abiria wangapi na balozi husika atapelekewa majina ya abiria wanaoelekea Nchini kwake," alisema Mkenda.
Nae Balozi mdogo wa Congo Nchini Tanzania alieko Kigoma, Nsenga Gaspara wamesaini Makubaliano hayo kwaajili ya kuepuka migogoro kwa wafanya biashara ya usafirishaji na wanaishukuri Serikali ya Tanzania kwa kutoa suruhisho kwa wafanya biashara kupata usafiri uliobora.
kwa Makubaliano hayo yatasaidia ukuaji wa uchumi kwa Wananchi wa Congo , Burundi na Tanzania kwa kuwa Nchi hizo zinategemeana kwa biashara na bidhaa mbali mbali za vyakula hivyo suala la usafiri ni la muhimu zaidi.
Aidha Mwakilishi wa Balozi wa Burundi Ininahazwe Albdert aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuliona hilo na kuweka makubaliano, na kuomba wafanya biashara watakao kiuka makubaliano hayo waitwe na kupewa utaratibu na waufuate pia ili kusaidia Wananchi wasikose usafiri na uwe salama.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...