Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, (Mb) wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema wananchi wa Chalinze,  wameweka historia ya kupata maji ya uhakika baada ya kuteseka miaka mingi kwa kukosa maji safi na salama.

Amewashukuru Rais John Magufuli na Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa wa Maendeleo walioufanya na hasa mchango wao kwenye mradi wa Maji wa Ruvu-Mboga.

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Polisi Chalinze, Mh. Kikwete alisema, “… namshukuru sana Hayati, Rais John Pombe Magufuli kwa kutupatia Shilingi bilioni 8 kwa ajili ya kuanzisha mradi huu wa maji. Pia Tunakushukuru wewe Mhe. Rais kwani ndani ya kipindi cha mwaka mmoja umeidhinisha Shilingi bilioni 11 na kufanya mradi huu kuwa na gharama ya Shilingi bilioni 19 ili mradi huu ukamilike mapema iwezekanavyo.”

Wananchi mbalimbali waohojiwa na mwanahabari wameshukuru hatua stahiki zilizochukiliwa na Mh. Rais hasa kutatua shida kubwa ya maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...