KAMPUNI ya vinywaji  ya TBL inayomilikiwa na kampuni ya AB Inbev imeendelea na jitihada  za kutafuta suluhu za  changamoto mbalimbali  za Maendeleo kwenye jamii kwa kwa kutoa wito kwa wavumbuzi kujiunga na Programu yao ya Accelerator 100+

Wito huo umetolewa leo Machi 31 2022 na Abigail Mutobiyerwa Meneja Masuala endelevu wa Kampuni ya TBL,  kwa wavumbuzi kutoka mikoa yote nchini kujiunga na Program hiyo ili kutafuta  suluhisho la changamoto  kwenye jamii kwenye ugavi, utunzaji wa vyanzo vya maji na  kilimo endelevu na mengineyo.

"Programu hii imedhamiria kuwezesha Kampuni ndogondogo zenye shauku ya kufanikiwa kwa kubuni na kuvumbua mawazo yenye tija kwenye jamii ili kutafuta suluhisho za changamoto za ugavi, utunzaji maji, kilimo, endelevu, mabadiliko ya tabia nchi, jkjaji wa pamoja na viumbe hai, amesema Abigail.

Amesema, katika miaka ya miwili iliyopita , programu hiyo imeziongezea uwezo kampuni 70 za kwenye nchi zaidi ya 20 na kuwajengea uwezo wajasiliamali wenye shauku kwa kuwasaidia kupeleka bidhaa zao sokoni kwa haraka.

Amesema kuwa rasmi TBL imefugua milango kwa kampuni chipukizi kwa ajili ya kujiunga kwa Program hiyo itakayowawezesha kupata mafunzo,Ushauri na pesa kiasi cha USD 100,000 kwa ajili ya kuendeleza miradi yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Chanzi Ltd, Andrew Wallace ambaye aliwahi kuwa mshindi wa programu hiyo ameshiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao na kusema  kupitia Accelerator 100+ wamekuwa wakikusanya chakula kinachotupwa na kukibadirisha kuwa chakula cha wanyama na mbolea halisi na kufanya kazi kubwa ya kuwezesha biashara nyingi kutafuta suluhisho za baadhi ya mambo ya kkmazungira yenye uharaka na changamoto za kijamii.

Aidha imeelezwa kwa waombaji wote watafanyiwa tathmini kwa awamu na salama zimetolewa ambapo mwisho kutuma maombi hayo ni tarehe 30 Aprili 2022 na kwamba maomb hayo yatumwe kupitia site ya www.100Accelerator.com

Meneja wa Masuala endelevu wa Kampuni ya TBL, Abigail Mutaboyerwa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza program ya 'Accelerator 100+' inayowezesha Kampuni chipukizi za kiuvumbuzi kutoka mikoa yote nchini kujiunga ili ziweze kupata Dola 100,000 za kimarekani ili kuziwesha kutatua changamoto za kimaendeleo endelevu katika nyanja za ugavi, utunzaji maji, kilimo endeleovu na mabadiliko ya tabia nchi. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Smart Lab, Edwin Bruno na Meneja Ugavi wa TBL, Dickson Rushekya.
Mkurugenz Mkaazi wa TBL, Jose Moran, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza program ya 'Accelerator 100+' inayowezesha Kampuni chipukizi za kiuvumbuzi kutoka mikoa yote nchini kujiunga ili ziweze kupata USD  100,000 zitakazowawezesha kutatua changamoto za kimaendeleo endelevu katika nyanja za ugavi, utunzaji maji, kilimo endeleovu na mabadiliko ya tabia nchi. Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Smart Lab, Edwin Bruno na Meneja wa Masuala endelevu wa TBL, Abigail Mutaboyerwa.
Meneja Ugavi wa Kampuni ya TBL, Dickson Rushekya akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza program ya 'Accelerator 100+' inayowezesha Kampuni chipukizi za kiuvumbuzi kutoka mikoa yote nchini kujiunga ziweze kupata Dola 100,000 za kimarekani ili kuziwesha kutatua changamoto za kimaendeleo endelevu katika nyanja za ugavi, utunzaji maji, kilimo endelevu na mabadiliko ya tabia nchi. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Smart Lab, Edwin Bruno na Meneja wa Masuala endelevu wa TBL, Abigail Mutaboyerwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...