WAKAZI tisa wa jjjini Dar es Salaam, wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka 746 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kujipatia zaidi ya sh. Bilioni 4.7 kwa njia ya udanganyifu.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Faraji Nguka imewataja washtakiwa hao kuwa ni wafanyabiashara Baraka Madafu, Bernad Mndolwa na Lusekelo Mbwele. Wengine ni Mark Mposo, Leena Joseph, Ofisa wa Benki Salvina Karugaba, Mohamed Kombo na Hussein Amani.
Aidha mahakama imelazimika kwenda kumsomea mashtaka, mshtakiwa Paul Shayo katika hospitali ya Kitengule Tegeta ambako amelazwa kwa matibabu.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ritha Tarimo wanakabiliwa na mashtaka 371 ya kughushi nyaraka na mengine 371 ya kuwasilisha nyaraka za uongo makosa ambayo waliyafanya
katika tarehe hizo hizo na maeneo hayo.
Akisoma hati ya mashtaka, Nguka amedai kuwa shtaka la kwanza linalowakabili washtakiwa wote ni kuongoza genge la uhalifu na kujipatia kiasi cha Sh 4,786,800,000 kosa wanalodaiwa kulitenda kati ya Aprili 1, 2019 na Desemba 31, 2020 katika Benki ya NBC tawi la Mnazi Mmoja, Ilala Dar es Salaam.
Washtakiwa hao pia wanadaiwa kujipatia sh. 4,786,800, 000/- kutoka benki ya NBC kwa udanganyifu baada ya kuwasilisha nyaraka za kugushi kuonesha kuwa watu 78 ni waajiriwa wa kudumu wa kampuni ya Peertech Company Limited na hivyo wanastahili kupewa mikopo wakati wakijua si kweli.
Aidha, washtakiwa wanadaiwa kutakatishaji kiasi hicho cha fedha, huku wakijua kuwa kosa hilo ni zao la kosa tangulizi la kughushi.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo uko katika hatua za mwisho na wako katika mchakato wa kufungua jalada katika Mahakama Kuu.
Baada ya kusomwa mashtaka hayo Hakimu Tarimo ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 13, 2022 na washtakiwa wote wamepelekwa mahabusu kwa kuwa shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...