Na.Khadija Seif, Michuzi TV.


WANAWAKE wenye Mafanikio wametakiwa kufanya jitihada na kutumia nguvu zao kuhakikisha Mabinti wadogo wanaziishi na kutimiza ndoto zao bila kupitia changamoto ya rushwa ya ngono na vitendo viovu.

Akizungumza na Michuzi TV Mbunifu wa Mavazi nchini kwa zaidi ya Miaka 10 Titty Moris amesema kupitia Sanaa yake ya Ubunifu wa Mavazi amehaidi kutimiza ndoto za wabunifu wachanga hususani Mabinti kwani anaamini wapo walio nyuma yake na ambao wanatamani kufika mbali hivyo kupitia wanawake waliofanikiwa na wenye ushawihi na nguvu katika jamii wakiungana Kwa pamoja wanaweza kutimiza ndoto za Mabinti wengi nchini.

"Lengo langu ni kuhakikisha wabunifu wachanga wanatimiza malengo yao katika sekta hii ya ubunifu, lakini tamasha hili litanogeshwa na wabunifu wachanga ambao wanafanya vizuri katika soko la mitindo nchini ila hawapata nafasi ya kuonekana ".

Titty Morris amesema anatarajia kufanya Tamasha la jukwaa la mitindo Marchi 19 mwaka huu katika Ukumbi wa Serena na kutakua na wabunifu mbalimbali Pamoja na watu Mashughuli lengo ni kufurahia Miaka 10 ya "Katty collection" na kufati a na zawadi aliyoiandaa Kwa wabunifu wachanga ikiwemo vyerehani

Tamasha hilo lenye lengo la tamasha hilo ni kutimiza miaka 10 katika tasnia ya mitindo, pia kukabidhi cherehani kwa wabunifu wachanga kwa ajili ya kutimiza ndoto zao.

" jukwaa hilo litapambwa na burudani mbalimbali za muziki, lakini wabunifu wawili wachanga wataonyesha mavazi yao ikiambatana na Ugawaji wa vyerehani Kwa wabunifu wachanga".

Titty ataonyesha Mavazi 10 ambayo yalipamba moto katika kipindi cha miaka 10 wakati ameingia kwenye Tasnia ya Mitindo.

"Nitaonyesha mavazi yangu 10 ambayo yalifanya vizuri kipindi chote ambacho nilianza fani hii, pia nitashiriki kubadilishana mawazo na wabunifu mbalimbali namna ya kukua katika soko la mitindo nchini".

Mbunifu huyo alitoa wito kwa wadau na taasisi kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo kwa ajili ya kushuhudia mavazi hayo.

Mbunifu wa Mavazi nchini kwa zaidi ya Miaka 10 Titty Moris "Katty collection" atoa ahadi ya kugawa vyerehani Kwa wabunifu wachanga na kusherehekea Miaka hiyo katika hafla maalum aliyoiandaa katika ukumbi wa Serena hotel inayotarajiwa kufanyika Machi 19 mwaka huu Jijini Dar es salaam.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...