Matukio mbalimbali katikati picha wakati maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakitoa elimu kuhusu athari za kufanya biashara za magendo maeneo ya mipakani.

Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kutembelea mipakani kutoa elimu kuhusu biashara za magendo kwa bidhaa ambazo zinazoingia na kutoka nchini Tanzania bila kufuata taratibu za kisheria.

Maofisa wa Forodha wametembelea mpaka wa Namanga pamoja na eneo la Mundarara Longido kwa ajili ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wanaozunguka maeneo hayo Mkoani Arusha.

Akitoa elimu hiyo Ofisa Msimamizi wa Kodi Julieth Kidemi amezitaja athari za magendo ikiwa nì kuhatarisha afya kwa watumiaji wa bidhaa zilizoingia kwa magendo bila kupitia maeneo yaliyoainishwa na Serikali kwa ajili ya ukaguzi na kupimwa kama zinafaa kwa matumizi ya binadamu.

Aidha ameongeza athari nyingine ya magendo nì uingizwaji wa vifaa ambavyo vinaweza kuwa na athari kwa usalama wa nchi ikiwemo mabomu na bunduki, hivyo kuhatarisha usalama wa Nchi.

Sambamba na hayo amewatahadharisha Wananchi kuacha kufanya biashara za magendo kwani kufanya hivyo kutasababisha kushuka kwa uchumi wa Nchi.

Pia alieleza adhabu za kisheria zitakazo chukuliwa kwa atakaye kamatwa na mzigo wa Magendo ambapo adhabu hizo ni pamoja na kifungo na faini.

Ametoa mwito kwa wananchi hao kutumia mipaka rasmi ambayo imeweka na Serikali katika uingizaji na utoaji wa mizigo, lengo likiwa ni kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo kutoka mamlaka husika zilizopo.

“Serikali inapowataka wananchi wapite kwenye mipaka rasmi sio kwa ajili ya kodi peke yake, maana kuna bidhaa nyingine hazilipiwi kodi, ila wanataka kwa ajili ya kupata takwimu Ili kujua kilichoingia na kutoka nchini “Amesema Afisa Kidemi.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Forodha Mkoa wa Arusha Paul Kamukulu ameshukuru kwa ujio wa Maafisa kutoka kitengo cha elimu kwenda kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wanaokaa maeneo ya mipakani kuhusiana umuhimu wa kupita mipaka iliyo rasmi, hivyo kwa elimu hiyo itawasaidia wananchi kuacha kuingiza bidhaa za magendo na kufata taratibu zilizowekwa na Serikali.

Nao baadhi ya wafanyabiashara waliopata elimu hiyo wameishukuru TRA, huku wakiomba Serikali kupunguza makali ya sheria za mipakani ili waweze kufanya biashara zao bila vizuizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...