KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imeridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa soko la wazi la wamachinga ulifikikia asilimia 67 na kuelekeza uongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha ujenzi huo unakamilikakwa wakati.
Akizungumza na wandishi wa habari jana jijini hapa mara baada ya ziara fupi ya kamati hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwini Mkanwa aliipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kwa kuwakumbuka wamachinga.
“Tumeridhishwa na ujenzi wa soko hili mnaenda vizuri sasa ni wajibu wahalmashauri ya jiji la Dodoma kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati ili wamachina wahamie hapa waendelee kufanya biashara zao kwa amani,”alisema
Mkanwa aliagiza halmashauri ya jiji la dodomakuzingatia viwango sahihi vya kodi ili kuepuka dosali ambazo zinaweza kujitokeza
“Tunataka muweke viwango rafiki kwa wamchinga msije mkaweka viwango ambavyo Rais, au Waziri Mkuu akija naye anashusha viwango mtakuwa mmedharirishwa hivyo ni bora mkaweka viwango rafiki ambayo havitaegemea upande wowote na katika hili ni vyema mkashirikisha wamachinga wenyewe,alibainisha
kwa upande wake katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga alisema ujenzi wa soko hilo la kisasa utasaidia kupendezesha jiji na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato.
Pili aliipongeza serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia kwa kugusa kundi kubwa la wamachinga ambao wamejiajili katika maeneo mbalimbali.
“Tumepata taarifa kuwa soko hili litakuwa na uwezo wa kuchukua wamachinga 2,938 ni watu wengi hivyo unategemea kuona baada ya kukamilika kwa soko hili jiji letulitakuwa safi na ongezeko la watu wanaolipa kodi,”alisema
Naye Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Francis Kaunda alisema kujengwa kwa mradi huo kutakuwa na faida nyingi kwa jiji la Dodoma, wafanyabiashara na Taifa kwa ujumla.
Alizitaja faida hizo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapato ambapo kukamilikakwa mradi huo jiji la Dodoma linatarajia kukusanya sh.bilion 1.1 kwa mwaka kutokana na kodi mbalimbali zitakazotozwa kwa baadhi ya huduma katika eneo hilo ikiwemo maegesho ya magari,vyoo, na mbao za matangazo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...