"CCM"
Showing posts with label CCM. Show all posts
NA WILLIUM PAUL, SAME.


ALIYEKUWA Mtia nia wa Ubunge katika Jimbo la Same mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi, CPA Ruth Hassan amewataka Wanachama wa Chama hicho katika Jimbo hilo kuvunja makundi na kuwapambania wagombea wanaotokana na CCM washinde kwa kishindo.

CPA Ruth alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Anna Kilango Malecel iliyofanyika katika kata ya Maore ambapo alisema kuwa, kwa sasa ndani ya chama wameshapatikana Wagombea wa kupeperusha katika nafasi ya Rais, Wabunge na Madiwani hivyo ni jukumu la wanaccm kuwa wamoja kuzitafuta kura.

"Natambua katika mchakato wa kura za maoni kila mmoja alikuwa na kundi lake lakini sasa ni muda wa makundi yote kuvunjwa na kuwa na kundi moja la CCM tuhakikishe Wagombea wetu wanapata kura za kishindo kuanzia Rais, Mbunge na Madiwani katika Jimbo letu" Alisema CPA Ruth.

Kada huyo wa CCM, alitumia pia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa jinsi walivompokea wakati amekuja kugombea na kudai kuwa CCM ni Chama chenye mchakato mzuri ya kuwachuja wagombea ili kumpata mmoja wa kupeperusha bendera na kupongeza kwa jinsi haki ilivyotendeka kuanzia vikao ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa.

CPA Ruth ambaye pia ni Mhasibu katika chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine ameahidi agenda yake ya kuhakikisha wananchi wa Jimbo hilo wanalima kilimo cha mkakati atashirikiana na Mbunge Anna pindi atakapochaguliwa kuhakikisha agenda hiyo inatekelezeka kwa vitendo.

"Wananchi tunawajibu wa kutambua kuwa mapinduzi ya kilimo yanapatikana ndani ya CCM hivyo nitashirikiana na Anna Kilango kuhakikisha kilimo chetu kinakuwa na nitaendelea kutoa elimu ya kilimo bure ndani ya Jimbo letu" Alisema CPA Ruth.

NA WILLIUM PAUL, SAME. 

MBUNGE mteule wa Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Anna Kilango Malecel amechukua fomu ya kugombea katika Jimbo hilo huku akitangaza kuvunja makundi ndani ya CCM. 

Anna Kilango alichukua fomu hiyo jana katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Same mashariki katika ofisi za halmashauri ya Same ambapo alisindikizwa na viongozi wa Chama wilaya pamoja na wanachama na wananchi wa same mashariki. 

Alisema kuwa, kwa sasa utaratibu ndani ya Chama umeshakamilika ambapo ameteuliwa kupeperusha bendera ya CCM na kuwataka wana CCM wote kuvunja makundi na kuwa na kundi moja la CCM kuhakikisha wagombea Udiwani, Mbunge na Rais wanashinda kwa kishindo. 

"Ninatambua wapo wanachama katika kipindi cha kura za maoni walikuwa hawaniungi mkono na ilikuwa ni haki yao kabisa maana wagombea wote tulikuwa wana CCM sasa jina limerudi moja la kwangu nawaombeni tuvunjeni makundi kuanzia sasa na tupambane kuhakikisha wagombea wa Chama chetu wanashinda kwa kishindo" Alisema Anna Kilango.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani akiongoza kikao cha Halmashuri Kuu ya CCM Taifa, ambacho kinafanya uteuzi wa mwisho wa majina ya Wanachama waliyoomba nafasi za Ubunge na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo na Viti Maalum leo Jumamosi Agosti 23,2025 mkoani Dodoma.


 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akiongoza kikao cha kawaida cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, leo Julai 14, 2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM (White House) mkoani Dodoma.

Kikao hicho, kinachotarajiwa kuendelea hadi Julai 16, kimeitishwa kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi wa nafasi za uwakilishi katika vyombo vya dola. Nafasi hizo zinahusisha ubunge wa majimbo, ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, viti maalum vya ubunge na Baraza la Wawakilishi, pamoja na udiwani wa kata na viti maalum.



 

 

Mtia nia James Innocent Mkinga (kulia), Mtaalamu mbobezi katika Fani ya Teknojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) akichukua fomu yake kuomba kuteuliwa kugombea jimbo hilo.

 

James Innocent Mkinga, Mtaalamu mbobezi katika Fani ya Teknojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

JOTO la Siasa katika Jimbo la Uchaguzi la Ludewa limezidi kupanda kufuatia kuendelea kujitokeza kwa watia nia mbalimbali wanaoashiria kuwepo kwa mchuano mkali jimboni humo. 

Jumapili Juni 29 2025, Mtia nia James Innocent Mkinga, Mtaalamu mbobezi katika Fani ya Teknojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Kada CCM na mwana harakati wa Maendeleo ya Vijana amejitokeza kwa mara ya pili kuchukua Fomu ili kushiriki katika mchakato wa kupata nafasi ya kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo hilo.


Na Mwandishi Wetu, Moshi
KADA  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Enock Koola (35), ambaye aliongoza katika kura za maoni katika kinyang’anyiro cha ubunge mwaka 2020, amechukua tena fomu ya kuwania tena nafasi hiyo ya uwakilishi, akiwa miongoni mwa waliojitokeza kumkabili mbunge anayemaliza muda wake Dkt. Charles Kimei.

Mapema leo Juni 28, 2025 saa 2 asubuhi, katika siku ya kwanza ya uchukuaji fomu za kuomba kuteuliwa na (CCM) kugombea ubunge, katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, Koola alikuwa mtia nia wa kwanza kufika katika Ofisi za CCM Wilaya ya Moshi na chukua fomu na kufuatiwa na washindani wengine watano, akiwamo Dkt. Kimei.

Wagombea wengine waliochukua fomu ni kuzirejesha leo kwa nyakati tofauti ni pamoja na Yuvenal Shirima, Diddas Lyamuya, Obrey Silayo na Lucy Mrema.

Baada ya kuchukua fomu katika Ofisi ya Katibu wa CCM, Wilaya ya Moshi Vijijini, Ramadhani Mahanyu kila mmoja kwa wakati wake, wagombea hao hawakuzungumza chochote na waandishi wa habari, badala yake kila mmoja alitoka na kwenda moja kwenye gari lake, kisha kuondoka.

Kivutio kikubwa katika uchukuaji na urejeshaji huo wa fomu walikuwa ni Koola na Dkt. Kimei, kutokana na ushindani mkubwa uliokuwapo baina yao katika kinyang’anyro cha mwaka 2020.

Itakumbukwa mwaka 2020 katika mchakato wa ndani wa chama, Koola ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi, alipata ushindi mbele ya wagombea wengine akiwamo Dkt. Charles Kimei ambaye ndiye aliyeteuliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho, kisha kushinda nafasi hiyo.

Koola ambaye ni msomi wa shahada ya uzamili (masters) alipata kura 187 kati ya 567 zilizopigwa, dhidi Dkt Kimei (ambaye alikuwa mshindani wake wa karibu) aliyepata kura 178 na kushika na nafasi ya pili. Wgombea wengine na kura zao kwenye mabano walikuwa Crisipin Meela (47), Laurance Mrack (44) na Regina Chonjo aliyepata kura 35.

Koola ni nani?
Katika siasa na uongozi, Enock mjumbe wa Baraza na mjumbe wa Kamati Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM ya mkoa wa Kilimanjaro (2022 – 2027) na pia Mjumbe wa Baraza hilo katika Wilaya Moshi Vijijini (2022 – 2027).

Kielimu, Enock ni msomi ambaye amepata elimu katika taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo Mei 2022 alipata cheti cha kuhitimu mafunzo ya Uongozi wa Bodi kutoka Institute of Directors Tanzania (IoDT), Dar es Salaam.

Kati ya Septemba 2010 hadi 2011 alisoma na kuhitimu masomo ya uzamiri (MSc) ya Usimamizi wa Uwekezaji (Investment Management) katika Shule Kuu ya Biashara ya Cass (Cass Business School), London nchini Uingereza

Kabla ya hapo, Septemba 2007 – Juni 2010, Enock alisoma na kuhitimu Shahada ya kwanza (BSc) katika masuala ya Usimamizi wa Fedha (Finance and Management) katika Chuo Kikuu cha Cardiff, nchini Uingereza.

Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni tatu; Gemini Engineering s Construction ya Dar es Salaam) tangu 2017, Hoteli ya Kilimanjaro Wonders ya mjini Moshi tangu 2015 na Kampuni ya A1 Outdoor Tanzania ya Dar es Salaam tangu 2014, Enock anatajwa kuwa mjuzi na mahiri katika uongozi wa biashara, usimamizi wa miradi mikubwa na midogo, uandaaji wa bajeti, uchambuzi wa kifedha, na usanifu wa mikakati.

Kadhalika aliwahi kuwa Afisa Mwandamizi wa Sapien Capital Limited ya London, Uingereza (Aprili 2012 – Disemba 2013.

Jimbo la Vunjo
Jimbo la Vunjo ambalo lipo Wilaya ya Moshi, lina hitoria isiyo rafiki kwa wabunge wanaomaliza muda wao, kwani hakuna mbunge aliyewahi kupata uwakilishi wa vipindi viwili mfululizo tangu lilipoanzishwa mwaka 1995, hivyo Dkt. Kimei ana kibarua cha kuvunja mwiko huo.

Jimbo la Vunjo kabla ya kuanzishwa kwake, lilikuwa sehemu ya Jimbo la Moshi Vijijini ambalo kwa takriban miaka kumi (1985 – 1990 na 1990 – Machi 1995 lilikuwa chini ya uwakilishi wa Augustine Mrema.

Mrema hakumaliza kipindi chake cha pili kwani alijiuzulu ubunge wake Machi 1995 na kuhamia NCCR Mageuzi baada ya kutofautina na achama chake hadharani.

Katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa Vyama vingi, jimbo hilo lilichukuliwa na James Mbatia kupitia NCCR Mageuzi, ambaye alifanikiwa tena kurejea katika nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kuwa mwakilishi mpaka 2020.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 ambao unatajwa kugubikwa na kasoro nyingi, Dkt. Kimei alichaguliwa kuwa Mbunge na anahitimisha uwakilishi wake Agosti 3, 2025.

Baada ya kufungua pazia la uwakilishi kupitia upinzani, katika Uchaguzi Mkuu wa 2000 Mbatia hakuweza kutetena nafasi yake na jimbo hilo, kwani lilitwaliwa na Meja Mstaafu, Jesse Makundi wa TLP (2000 -2005) ambaye pia alikaa kwa kipindi kimoja tu.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, Meja mtaafu Makundi hakurejea kwani Vunjo walimchagua Aloyce Benti Kimaro (sasa ni marehemu) kupitia CCM kuwa mbunge wao kwa kipindi cha 2005 - 2010.

Kimaro baada ya kumaliza kipindi chake naye hakufanikiwa kurejea tena kwani Katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Augustino Mrema alichaguliwa kuwa Mbunge akiliwakilisha bungeni Jimbo la Vunjo kati ya 2010 – 2015. Mrema pia hakurejea kwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Mbatia alirejea tena Vunjo.
Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, imekutana katika kikao chake maalum leo Jumamosi tarehe 28 Juni 2025, kufuatilia mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi ndani ya CCM. 

Kikao hicho kilipokea na kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali za zoezi hilo la uchukuaji wa fomu za kuwania uteuzi wa kugombea nafasi za uwakilishi katika vyombo vya dola, lililoanza rasmi leo kwa mchakato wa ndani ya CCM, katika maeneo yote nchi nzima. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali, ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu hizo za kuwania kuteuliwa ndani ya CCM, imeanza leo tarehe 28 Juni 2025, saa 2:00 asubuhi na itahitimishwa tarehe 2 Julai 2025, saa 10:00 jioni.
Ratiba hiyo itahusisha uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi nafasi za; Ubunge wa Jimbo, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ubunge wa Viti Maalum, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum, Udiwani wa Kata au Wadi na Udiwani wa Viti Maalum. 




 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amechukua fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Rombo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Rombo, Massoud MeliMeli



 

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV-Katoro

MAKAMU Mweyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira ametaja mambo manne muhimu ambayo Chama kitaendelea kuyatekeleza kwa nguvu zote kwa mustakabali wa taifa.

Wasira ameyasema hayo jana Juni 17, 2025 alipokuwa akizingumza na wana CCM katika mkutano wa hadhara Katoro, mkoani Geita akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama mkoani humo ambapo pia amefanya vikao vya ndani.

Amesema jambo la kwanza ambalo CCM itaendelea kusimamia kwa nguvu zote ni umoja na mshikamano wa Watanzania ambapo alisema fafanua msingi wa umoja una mkono wa watu ambao tayari wametangulia mbele ya haki.

“Kuna wazee nyuma yetu ambao wametangulia mbele ya haki wametuachia kazi hiyo tuiendeleze, wapo wazee kama Mwalimu Julius Nyerere, Hayati Abeid Aman Karume ambaye alikubali kuacha urais wa nchi yake awe Makamu wa Rais kwa sababu ya umoja wa taifa,” amesema.

Wasira alitaja jambo la pili muhimu kwa Chama ni kusimamia amani iliyopo na kueleza kuwa sasa kuna baadhi ya watu wanachezea amani iliyopo ikiwemo kupanga kuvunja Katiba wazuie uchaguzi.

Aliwaeleza wananchi hao kuwa, yeyote anayewaambia wamuunge mkono kuchukua hatua ambazo ni kinyume na Katiba wakatae. “Ninawaambia ajenda ya amani ni ajenda yetu, tena ni ajenda ya kudumu kwa chama cha kudumu.”

Jambo la tatu alisema ni CCM kuendeleza uhuru wa taifa kwa kuwa ndio unasaidia kufanya uamuzi na kufafanua kuwa wananchi waliudai ili kuamua mambo yao wakiwa huru.

Alitaja jambo la nne ni kuendelea kuleta maendeleo ya Watanzania na katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa, nzuri kusimamia maendeleo.






Na Mwandishi Wetu,Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa wito kwa wanawake nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia katika mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama hadi uchaguzi mkuu wa dola Oktoba 2025.

Hayo wakati akizungumza na Kikundi cha Wanawake wa Kikiristo na Maendeleo Zanzibar kanda ya Magharib ‘B’ huko Kiembesamaki Unguja.

Dkt.Dimwa, amesema CCM inatambua mchango mkubwa wa wanawake katika ustawi wa jamii na maendeleo ya nchi.

Alisema maendeleo yaliyofikiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi yamechangiwa na nguvu kazi ya Wanawake wanaosimamia kikamilifu masuala mbalimbali ya kisiasa na kimaendeleo.

“Natoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wana uwezo wa kuleza mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Dhamira ya chama cha mapinduzi ni kuhakikisha wanachama wote wanapata haki na fursa sawa katika kuimarisha demokrasia.”alisema Dkt.Dimwa.

Aidha, alieleza kuwa kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, chama hicho kimeweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha wanawake kwa njia mbalimbali, ikiwemo mafunzo ya uongozi, uwezeshaji kiuchumi, na kuhamasisha ushiriki wao katika siasa.

Alitoa mfano wa wanawake walioshiriki harakati za kupigania maslahi ya CCM toka wakati wa ASP na TANU ambapo aliwataja waasisi hao ambao ni Bibi Titi Mohamed,Bi.Johari Yussuf Akida na Bi.Mwanaidi Dai.

Katika hotuba yake, Dkt. Dimwa pia alizungumzia umuhimu wa kupinga vitendo vya ubaguzi wa kidini na kikabila, na kuahidi kuwa CCM itaendelea kusimamia haki na usawa kwa wanachama wake wote.

Alisema kuwa chama kinaendelea kudhibiti vitendo vya rushwa ili kuhakikisha kila mwanachama anapata haki anayostahiki kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya Chama hicho.

Alisisitiza umuhimu wa wananchi kulinda amani na utulivu uliopo nchini ili kuhakikisha uchaguzi mkuu wa dola wa mwaka 2025 unafanyika katika hali ya amani.

Alisema CCM itapata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 uliofanywa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali ya awamu ya nane chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi.

Naye Mwenyekiti wa Kikundi hicho,Catherine Peter Nao alieleza kuwa wataendelea kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wanawake mbalimbali nchini kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi nchini.

Catherine,aleleza kuwa wamejipanga kuhamisha na kutangaza maendeleo yaliyotekelezwa na serikali zote mbili ili wananchi waweze kujua kazi zinazofanywa na serikali iliyopo madarakani.

Caption.

Picha no.99 na 77- NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa,akizungumza na kikundi cha Wanawake wa Kikiristo na Maendeleo kanda ya Magharib “B”.

Picha no.44-Picha ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, pamoja na Viongozi wa Kikundi cha Wanawake wa Kikiristo Zanzibar.Picha na Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga, Sinzo Mgeja,

Na Mwandishi Wetu
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga, Sinzo Mgeja, amewaasa vijana nchini kutokubali kutumika na baadhi ya wanasiasa kuhamasisha uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, badala yake wawe mstari wa mbele kuilinda.

Sinzo alisema hayo jijini Dar es Salaam, jana, alipozungumza na gazeti hili kuhusu nasaha kwa vijana kuelekea uchaguzi mkuu.

Alisema vijana ndiyo taifa la kesho, hivyo kamwe wasikubali kutumika kama chanzo cha machafuko kwa taifa, badala yake wawe mfano wa kuigwa katika suala zima la kuhubiri amani.

Sinzo alisema jukumu la kulinda amani siyo la mtu mmoja, bali ni la kila Mtanzania wakiwemo vijana ambao ni tegemeo la taifa.

“Tanzania inasifika duniani kuwa ni kisiwa cha amani. Amani hii inapaswa kuendelea kuwepo kizazi hadi kizazi na wanasiasa wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuilinda amani hiyo,”. alisema.

Sinzo alieleza vijana wanatakiwa kuutanguliza uzalendo na kuachana na baadhi ya wanasiasa hao ambao wanatanguliza maslahi yao binafsi.

Pia, aliwaomba vijana kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi, kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM akiwemo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani.

“Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 inaonesha vijana wapo milioni 21. 3 kati ya watu milioni 61. Kutokana na takwimu hizo vijana wana nafasi kubwa ya kuungana pamoja kuwakataa wanasiasa wanaotaka kuwarubuni na kuwashawishi kushiriki katika vitendo visivyofaa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu," alisema

Kada huyo aliwaomba Watanzania wakiwemo vijana kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu kwa kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM.

Sinzo aliwaomba watakaopata fursa ya kuchaguliwa kuwa viongozi kuendelea kuilinda amani na kufanya kazi kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu.

Mbali na hayo, Sinzo aliwaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia na kuhakikisha wanampa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu.

  Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiburudika burudani ya mziki kutoka Kikundi cha Sanaa cha Tanzania One Theatre (TOT), kikiongozwa na Malkia wa Mipasho na Mziki wa Taarab, Bi. Khadija Omar Abdallah Kopa, leo Ijumaa tarehe 30 Mei 2025, jijini Dodoma. 


Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa huo ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ulianza jana Alhamis, tarehe 29 Mei 2025, na leo unaendelea katika siku yake ya pili, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, ambapo mojawapo ya agenda itakuwa ni kuzindua Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025 - 2030. 








 

Mwamvua Mwinyi, Rufiji Mei 6,2025

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Mary Chatanda, amepokea mradi mkubwa wa vifaa vya ujasiriamali wa upishi na gari jipya kwa ajili ya kuimarisha utendaji wa UWT Mkoa wa Pwani kutoka kwa Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, Hajat Mariam Ulega. 

Mradi huo ambao umetolewa na Mbaraza huyo mei 6,2025 ambapo umejumuisha gari aina ya Alphard (G) lenye namba za usajili T 912 ELT, pamoja na vifaa vya kisasa vya upishi ikiwemo sahani za udongo 200 ,vikombe vya chai 200 ,bakuli za supu 200,Glass za udongo 200 na saving dish 10.

Pia Mama Ulega alitoa majiko mawili ya gesi ya kisasa,sufuria kubwa 12,madeli 2,chupa za chai 4,miko 8,Mbakuli mikubwa ya udongo 10 na matray 4 ya kubebea vyombo

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, katika ziara yake aliyoianza mkoani Pwani, Chatanda aliipongeza UWT Mkoani humo kwa kazi kubwa na ubunifu katika kuimarisha jumuiya.

Alisisitiza kuwa ,mradi huo wa kiuchumi utaongeza tija na kuimarisha miradi ya maendeleo inayowahusisha wanawake katika mkoa huo.

Aidha, Chatanda alihimiza mshikamano na kuwataka wanachama wa CCM kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao, wakihakikisha ushindi mkubwa kwa chama na kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Umoja wetu ndio msingi wa ushindi wetu, Tuimarishe mshikamano wetu na tuhakikishe Dkt. Samia anapata kura za kishindo, kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa," alisema Chatanda. 

Awali akikabidhi vifaa hivyo Mariam Ulega alieleza , kutoa ni mazoea moyo kila mtu anao. 

Alifafanua , gari hiyo itasaidia kuzisaka kura za Rais Dk Samia na ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu. 

Mapokezi ya Chatanda huko Rufiji yalipambwa na hamasa kubwa kutoka kwa wananchi na viongozi wa chama, akiwemo Mwenyekiti wa UWT Mkoa, Zainabu Matitu Vulu, Mkuu wa Mkoa Abubakary Kunenge, Waziri wa TAMISEMI na MNEC wa Mkoa Mohamed Mchengerwa, Wabunge wa Viti Maalum pamoja na viongozi wa kisiasa na serikali kutoka mkoa wa Pwani.





 

LEO Aprili 29, 2025, wanachuo na wakufunzi wao kutoka Chuo Kikuu Cha Whitworth cha Marekani, wametembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Katibu wa NEC Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid.

Pamoja na mambo mengine, wanachuo hao wanaosoma masomo ya siasa, falsafa na uhusiano kimataifa, walitaka kupata ufahamu juu ya masuala ya demokrasia, sera za CCM kuhusiana na watu wenye ulemavu, miundombinu na maendeleo ya watu kwa ujumla

Wanachuo hao wapo nchini kwa kushirikiana na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kivukoni, Dar es Salaam kujifunza utamaduni wa Tanzania, lugha ya Kiswahili pamoja na mafunzo kwa vitendo.






Mwamvua Mwinyi, Kibaha Aprili 25, 2025

SPIKA wa Bunge na Rais wa 31 wa Muungano wa Mabunge Duniani IPU ,Dkt. Tulia Ackson, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini, mkoani Pwani, kuacha ushindani na makundi ndani ya chama,  ambao unaweza kusababisha madhara kwa kutoa upenyo kwa upinzani wakati wa Uchaguzi. 

Aidha Dkt. Tulia aliwaambia wanachama wakati wa Uchaguzi ukifika wachague viongozi wanaowafaa na bora badala ya kuchagua wale wenye nia ya kutaka kujaribu.

Akizungumza April 25,2025 na viongozi ,mabalozi pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kibaha Mjini, kutoka kata ya Viziwaziwa,Kongowe na Msangani wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, Dkt Tulia ambae alikuwa mgeni maalum aliongeza, waachane na ushindani ili kukiimarisha Chama.

"Msifanye ushindani wa namna ya Yanga na Simba, bali muangalie viongozi ambao wanaonekana kufanya kazi kwa manufaa yenu".  

Vilevile Tulia anabainisha, Kibaha Mjini haipo kinyonge, ilani ya utekelezaji ya CCM imetekelezwa kwa kiasi kikubwa. 

" Wanaccm lazima tuwatupe mbali wapinzani, utekelezaji unaonekana kwa macho, Rais Samia Suluhu Hassan anastahili heshima kwa kumpa kura za ushindi na sio za kinyonge." 

Nae mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati Kuu na Mlezi wa Mkoa wa Pwani, Leilah Ngozi  alisema wanachama wanaojipitisha kwa kufanya kampeni kabla ya wakati, wakemewe bila woga na kufikishwa kwenye vikao vya kimaadili.

Pia aliwakumbusha viongozi kuzingatia haki katika kufanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za Uongozi katika mchakato wote wa uchaguzi.

Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, alieleza mafanikio yaliyopatikana bungeni, akisema kuwa asilimia 97 ya maswali na majibu yaliyoulizwa bungeni yametekelezwa. 
"Naishukuru serikali kwa kutatua kero mbalimbali kupitia sekta ya afya, maji, elimu, barabara ambazo nilizozifikisha bungeni na nyingine zinatekelezwa na serikali kuu," alisema Koka.

Koka anajivunia kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM, akisisitiza kuwa anajivunia hatua zilizofikiwa, ikiwemo kushirikiana na viongozi wa wilaya kupigania halmashauri ya Mji kuwa na hadhi ya Manispaa. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini, Mwl. Mwajuma Nyamka alieleza , mji huo una kata 14 ,wajumbe wa mkutano huo ni 8,000 ,mikutano itafanyika kwa siku tano kuanzia April 23- 27 ambapo kila siku zitashiriki kata tatu .