Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wanawake
na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanawake
wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa
Shinyanga wamesherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa mahitaji
mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi mahitaji hayo leo Ijumaa Machi 11,2022 katika wodi
za wanawake na watoto, Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga,
Amina Mdabi amesema wamefika katika hospitali hiyo ili kutoa faraja kwa
wanawake na watoto ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya Wanawake
Duniani ambayo husherehekewa ulimwenguni kote Machi 8.
“Sisi
wanawake kutoka NSSF Shinyanga tumekuja hapa kusherehekea siku ya
wanawake duniani na wanawake ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Shinyanga kwa kuleta mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni za
unga na miche, mafuta ya kujipaka,pipi,biskuti, maji na juisi”,amesema Mdabi.
Naye
Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,
Victoria Mmasy akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali
hiyo amewashukuru wanawake hao kwa kufika katika hospitalini hapo na
kutoa mahitaji kwa akina mama na watoto waliolazwa.
Nao
akina mama waliolazwa katika hospitali hiyo wamewashukuru wanawake hao
kutoka NSSF mkoa wa Shinyanga kwa kuwapatia mahitaji hayo ambayo
yatawasaidia katika kipindi hiki wakiendelea kupatiwa huduma za matibabu
hospitalini hapo.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi akizungumza wakati Wanawake
wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa
Shinyanga wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto
waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni
sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani leo Ijumaa Machi
11,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (wa nne kulia) akizungumza wakati Wanawake
wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa
Shinyanga wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto
waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (kushoto) akizungumza wakati Wanawake
wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa
Shinyanga wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto
waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Sehemu
ya mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni za unga na miche, mafuta ya
kujipaka,pipi,biskuti, maji na juisi vilivyotolewa na Wanawake
wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga kwa wanawake na watoto waliolazwa
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akikabidhi sabuni ya unga na mahitaji mengine kwa Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (wa nne kulia) kwa ajili ya wanawake
na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akikabidhi sabuni ya unga na mahitaji mengine kwa Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (wa nne kulia) kwa ajili ya kwa
wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani.
Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (katikati) akiangalia mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na Wanawake
wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa
Shinyanga kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Shinyanga
Wauguzi
na wanawake wafanyakazi NSSF Shinyanga wakijiandaa kugawa mahitaji
mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake
duniani
Wauguzi
na wanawake wafanyakazi NSSF Shinyanga wakijiandaa kugawa mahitaji
mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake
duniani
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi akikabidhi mafuta ya kujipaka kwa mmoja wa wanawake wodini. Kila mwanamke wodini amepatiwa mafuta,sabuni ya unga na mche,juisi, pipi na maji.
Afisa
Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi akikabidhi
mafuta ya kujipaka kwa mmoja wa wanawake wodini. Kila mwanamke wodini
amepatiwa mafuta,sabuni ya unga na mche,juisi, pipi na maji
Wanawake NSSF Mkoa wa Shinyanga wakimwangalia mtoto aliyelazwa wodini wakati wakikabidhi mahitaji mbalimbali.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akikabidhi sabuni na mafuta kwa mmoja wa wanawake wodini
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akizungumza na mama anayeuguza mtoto wake wodini
Wanawake wafanyakazi NSSF Mkoa wa Shinyanga wakiwa wodini
Zoezi la kukabidhi mahitaji mbalimbali wodini likiendelea
Zoezi la kukabidhi mahitaji mbalimbali wodini likiendelea.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...