Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Polio nchini Malawi,katika kuchukua tahadhari mko wa Njombe unaopakana na nchi hiyo unatarajia kutoa chanjo ya matone kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wapatao 110,173 ili kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo amesema watoto watapata chanjo hiyo bila kujali kama walishapata chanjo hiyo katika ratiba zao za awali.

“Kampeni hii inalenga kutoa chanjo kwa jumla ya watoto laki moja elfu kumi na mia sabini na tatu katika mkoa wetu wa Njombe aidha watoto wote chini ya miaka mitano watapata chanjo bila kujali walishapata chanjo hii katika ratiba zao za kawaida za chanjo”alisema Kissa Kasongwa

Aidha amesema serikali ya Tanzania inatarajia kutoa chanjo ya kuzuia ugonjwa huo usio kuwa na tiba kwa mikoa yote nchini kwa kuanza na mikoa iliyo karibu nan chi ya Malawi amabyo ni mkoa wa Njombe,Ruvuma,Mbeya na Songwe.

Bi,Kissa ametoa wito kwa wananchi wote kupokea kampeni hiyo inayotarajiwa kuanza hapo kesho March 24 mwaka huu ili kujikinga na ugonjwa huo wenye madhara makubwa.

“Madhara makubwa ya ugonjwa wa polio ni ulemavu wa ghafla wa viungo na huathiri zaidi watoto walio na umri chini ya miaka 15”amebainisha Kaongwa

Vile vile amebainisha sababu za ugonjwa huo.

“Ugonjwa wa polio unasababishwa na kirusi cha Polio ambacho huambukizwa kutoka kwa mtu aliyeathirika kwenda kwa mwingine kwa kunywa au kula chakula au kinywaji kinachochafuliwa kwa kinyesi chenye vimelea vya ugonjwa wa polio,virusi vya Polio huzaliana katika utumbo na huweza kuathiri mfumo wa fahamu ikiwa ni pamoja na kupooza kwa ghafla kwa viungo ndani ya masaa machache hata kupelekea kifo”alisema Kissa

Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Zabron Masatu amesema hata kama mtoto alikwishapata chanjo hiyo hakuna madhara yeyote yatakayopatikana kwa kupata chanjo kwa mara nyingine.

“Hata kama mtoto alipata chanjo ana kinga nab ado ataongewzewa tena kinga na tunachnja watoto wote kuhakikisha hatumuachi hata mtoto mmoja na tunatambua katika hawa kuna wengine walishachanja lakini wapo wengine hawakuchanja ila kwasababu tuko kwenye hatari lazima tuhakikishe mtoto ambaye yupo chini ya umri wa miaka mitano anachanjwa”alisema Masatu

 

 Kissa Kasongwa mkuu wa wilaya ya Njombe akitoa taarifa ya kuanza kutoa chanjo ya Polio kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Waziri Kindamba.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...