Janeth Raphael - MichuziTv
Inaelezwa kuwa watu zaidi ya milioni 253 Duniani wana matatizo ya kutokuona vizuri.
Hayo yamezungumzwa leo Machi 7, 2022 Jijini Dodoma na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt Aifelo Sichalwe wakati akizindua wiki ya maadhimisho ya shinikizo la macho Duniani.
Dkt Sichalwe amesema kati ya wagonjwa hao 253 wenye matatizo ya macho milioni 36 hawaoni kabisa, zaidi ya 75% ya visababishi vya kutokuona vizuri vinaweza kuzuilika na kutibika kabisa.
"Asilimia 2.8 ya watu wote wenye upungufu wa kutokuona vizuri ambao ni sawa na watu milioni 7. 7 duniani kote wana ugonjwa wa shinikizo la macho na kati yao milioni 4. 2 hawaoni kabisa" - Amesema Dkt Sichwalwe.
Dkt Sichwalwe Amesema Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa, Duniani itakapofika mwaka 2040 kutakuwa na watu wenye shinikizo la macho zaidi ya watu milioni 114, ongezeko hilo ni kubwa hivyo zinahitajika juhudi za makusudi kuhakikisha kwamba watu wanagundulika mapema na Kupata matibabu kwa wakati.
"Asilimia 90 ya watu ambao wako huko kwenye jamiii wenye matatizo ya shinikizo la macho hawajagundulika kabisa na hawajafika kwenye vituo vya afya kabisa" - Dkt Sichwalwe
Hata hivyo Dkt Sichwalwe amesema ili kupunguza uwezekano wa kupata madhara au Kupata ugonjwa huo wataalamu wanashauri kuacha matumizi ya kunywa dawa holela na dawa za wagonjwa wengine hata hujapima unaanza kutumia hizo dawa, ni muhimu kufata wataalamu wanavyoelekeza.
" Hivyo nahimiza na kuwaagiza wataalamu wote nchini kuzingatiwa mwongozo wa Taifa wa tiba ya mwaka 2021 kwa matumizi sahihi ya dawa" Amesema Dkt Sichwale.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mpaka Dkt Alphonce Chitanda amesema ugojwa huo wa shinikizo la macho ni moja kati ya kundi la magonjwa ya macho yanayoshambulia mishipa ya fahamu wa kuonea, na ni ugonjwa hatari unaoadhiri uoni kwa taratibu sana siku hadi siku bia dalili yoyote.
"Ugonjwa huu unaadhiri macho pole pole pasipo kufahamu na unaweza kujiona uko sahihi hauna shida yeyote kumbe presha ya macho iko juu na mshipa wa fahamu kuendelea kuashirika na kuja kugundulika wakati huwezi kuona kwa hiyo ugonjwa huu ni Kama mwizi wa kimya kimya wa wezi wa macho kuona " - Dkt Chandika.
Dkt Chitanda amesema wao Kama wadau wa afya inabidi kuupa kipaumbele Sana ugonjwa huo kwa sababu unaadhiri nguvu kazi ya Taifa na kupelekea Taifa ambalo wananchi wake hawataweza kuona vizuri na kuadhiri uzalishaji.
Hata hivyo kwa takwimu za kitaalamu ugonjwa huo inainyesha unaadhiri zaidi watu wenye umri wa miaka kuanzia 40 na kuendelea, hivyo hao ni kundi ambalo linadhirika zaidi, ni vyema kuhakikisha kwamba watu hao wanachunguzwa afya zao za macho Mara kwa mara.
Naye mgonjwa wa presha ya macho anayetibiwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa Jenipha Mrema amesema amejigundua ana presha ya macho miaka 9 iliyopita na katika miaka hiyo tisa amekuwa akihudhuria kiliniki ya matibabu hayo hospitalini hapo na anaishukuru hospitali hiyo kwani wamekuwa karibu naye sana.
"Nawashauri Wana jamii wenzangu msiache kupima presha ya macho kwa sababu ni ugonjwa ambao hauna dalili huwezi kusema leo nina kichefu chefu labda nipime maleria hapana, hivyo mpaka unakuja kushituka unaenda kupima unakuwa umeadhirika pakubwa" - Amesema Jenipha.
Jenipha ameishukuru Serikali kwa kuwa hapo mwanzo Kupata dawa ilikuwa changamoto lakini kwa Sasa kila akifika hospitalini hapo dawa zinapatikana kwa wingi na kila anapohitaji anapewa.
Hata hivyo Jenipha ametoa wito kwa kila anayeugua ugonjwa huo kuelimisha jamii kwani hata anayemsinsikiza mgonjwa hospitalini awe anaangalia afya yake kwa sababu naye inawezekana hayuko salama.
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt Aifelo Sichalwe wakati akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani)
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt Alphonce Chitanda
Mgonjwa wa presha ya macho anayetibiwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa Jenipha Mrema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...