Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

KATIBU Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael amefanya mazungumzo na watumishi na viongozi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) huku akitumia nafasi kupongeza chuo hicho kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao vema na kuwambusha kwamba jambo nzuri kwa watumishi wa umma ni kuchapa kazi kwa nidhamu ya hali ya juu

Dk.Michael amesema hayo baada ya kufanya ziara katika Chuo hicho ikiwa ni sehemu ya kuzitekeleza taasisi,idara na mashirika yaliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.Akiwa katika Chuo hicho amejionea shughuli za chuo hicho.


"Jambo kubwa katika utumishi wa Umma ni kuchapa kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kwa weledi na kwa juhudi kubwa , kufuata miongozo na taratibu zilizopo, kutii viongozi sambamba na kutumia muda mwingi kwenye kazi.Lakini naomba niseme Chuo hiki kina bahati ya kuwa na watumishi wengi vijana wanaofanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu,"amesema.

Ametumia nafasi hiyo kuutaka uongozi wa Chuo hicho kuwatafutia nafasi za masomo watumishi hao ili kujiendeleza na kwamba kwa kufanya hivyo kutaongeza morali ya kazi kwa watumishi hao na kufanyakazi kwa bidii na weledi.

"Hapa naona kuna damu changa, kuna wakufunguzi wengi wadogo nikuombe Mkurugeni kuwatafutia nafasi za masomo wajiendeleze kimasomo, wapelekeni kwenye masomo kwani kusomesha watumishi ni kazi ya Taasisi, kuna faida kubwa ikiwemo kumfanya mtumishi aipende Taasisi

"Hivyo nikuombe sana Mkurugenzi tafuta fedha na mimi nitakusaidia kutafuta ili hawa watumishi waende shule wakirudi utakuwa umeongeza motisha ya kazi na kuendelea kuipenda kazi yao na kuifanya Taasisi kuwa na wataalamu wa kutosha na hivyo kufikia malengo yake"ameongeza Dkt. Michael.

Awali akitoa hotuba ya utangulizi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka ameelezea kazi mbalimbali za utoaji mafunzo zinazofanywa na Chuo hicho katika Kampasi zake nne ikiemo Bustani iliyoko katikati ya Jiji la Dar es Salaam, Temeke, Arusha na Mwanza, na kwamba kwa sasa Chuo hicho kinaendelea na jitihada zake za kuhakikisha kinapata watumishi wa kutosha kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kukiwezesha Chuo kuendelea na mipango yake mbalimbali.

Aidha amesema katika mwaka huu wa fedha Chuo hicho kimekuwa na vipaumbele saba ambavyo mpaka sasa ndio majukumu yao wanayoendelea kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kuimarisha mafunzo na shughuli za chuo hicho.

Amesema katika mwaka huu wa fedha wamekuwa na vipaumbele ambavyo ni pamoja na kuimarisha kampasi yetu mpya iliyopo kule mwanza, kuandaa sheria mpya ya uendeshaji wa chuo, kuongeza wigo wa kukusanya mapato ili kupunguza utegemezi kutoka Serikali Kuu.

Pia walikuwa na kipaumbele cha kuongeza uwezo wa kufanya utafiti katika Sekta ya Utalii na Ukarimu."Pia tuna lengo la kupanua Kampasi yetu ya Arusha ambapo kimkakati Arusha ndio Mkoa unao ongoza katika shuguli za Utalii, lengo letu lingine ni kuhamisha Kampasi yetu ya temeke iliyopo kwenye Wilaya ya Temeke."

Pia Dkt. Sedoyeka amemueleza Katibu Mkuu huyo changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo uhaba wa watumishi katika maeneo mbalimbali, changamoto ya Chuo kutokuwa na Muundo wake, miundombinu chakavu, madeni ya ndani na nje ya muda mrefu,ufinyu wa bajeti .

Ambapo ameeleza kuwa changamoto hii imefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa na katika mwaka huu wa fedha Chuo kimepata fedha kwa wakati hivyo kuishukuru Serikali na kwamba ana imani kubwa kwa mwaka ujao wa fedha wataongezewa fedha katika bajeti yao.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael akizungumza na watumishi wa na viongozi wa chuo cha taifa cha Utalii (NCT) alipofanya ziara Chuoni hapo kujionea shughuli za chuo hicho na kuzungumza na watumishi ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoifanya ya kutembelea Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Watumishi wa Chuo cha Taifa Utalii wakifuatilia ootuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael
Mkurugunzi wa Fedha na Utawala wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) CPA Munguabela Kakulima akizungumza wakati alipokuwa akifanya utambulisho katika mkutano huo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya utangulizi katika mkutano huo uliofanyika katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam .
 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prisca Rwangila (kulia) wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prisca Rwangila (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Chuo cha taifa cha Utalii (NCT) CPA. Munguabela Kakulima mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Jijini Dar es Salaam


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...