Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ameshuhudia utiaji saini wa mkataba baina ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wa Mkoa wa Lindi na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Limited kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji safi na salama wa mradi wa Nnyangao - Mtama
Ujenzi wa mradi huo utanufainisha na kuwawezesha wananchi zaidi ya 22,000 kupata maji safi na salama ambao utagharimu zaidi ya shilingi 4,577,244,446
Mradi huo utatekelezwa jimboni humo kwenye kata tatu za Majengo, Mtama na Nyangao zenye jumla ya vijiji 13 vya Nyangao A, Nyangao B, Mtakuja II, Nangaka, Masasi, Majengo A, Majengo B, Mvuleni, Mihogoni, Mbalala, Makonde, Mnamba (Chluwe) na Mkwajuni
Viongozi wengine walioambatana na Mhe. Waziri Nape ni Mhe. Shaibu Issa Ndemanga, Mkuu wa Wilaya Lindi; Mhe. Yusuph Abdalah Tipu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama; Waheshimiwa madiwani wa maeneo husika, watendaji wa Ruwasa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti comred Athumani Seif Hongonyoko.
Waziri Nape amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akifurahia na baadhi ya Wananchi wa jimboni kwake mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi mradi wa maji safi na salama baina ya RUWASA na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Ltd kwa ajili ya kufikisha huduma ya maji kwenye kata tatu za jimbo hilo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...