Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo Machi 29 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori
Katika mazungumzo hayo Waziri Dkt.Ndumbaro amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuweka mazingira rafiki ya Uwekezaji kwa Wawekezaji wa kutoka Marekani hususani katika sekta ya Uwindaji wa Kitalii kwa kuzingatia maslahi ya nchi
" Moja ya shabaha yetu kama Wizara ni kuwavutia Wawekezaji, tunafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha Wawekezaji wa kutoka nchi mbalimbali wakiwemo wa Marekani wanawekeza katika uwekezaji huu wa muda mrefu'' amesisitiza Dkt. Ndumbaro
Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kukusanya Sh23 bilioni kwa mwaka kutokana na uwekezaji mahiri unaoendekea kufanywa kwenye sekta ya utalii nchini

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam Picha na WMU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akiagana na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright mara baada ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam Picha na WMU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam Picha na WMU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...