Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP Suleiman Mzee, akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Jeshi hilo leo, inayojengwa Msalato jijini Dodoma. Waziri Masauni alifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya jeshi hilo itakayotembelewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia meza kuu), akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP Suleiman Mzee, alipokuwa anawasilisha taarifa ya miradi mbalimbali kwa Waziri huyo wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Jeshi hilo, Msalato jijini Dodoma, leo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiwa katika kikao na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu ya Jeshi hilo, wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Jeshi hilo, Msalato jijini Dodoma, leo, itakayotembelewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Baadhi ya nyumba za makazi ya askari wa Jeshi la Magereza zitakazozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Msalato, jijini Dodoma hivi karibuni. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Jeshi hilo kabla ya ujio wa Rais. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP Suleiman Mzee, ofisini kwa Mkuu wa Jeshi hilo leo, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya jeshi hilo itakayotembelewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP Suleiman Mzee (kushoto), kabla ya kuanza ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya Jeshi hilo itakayotembelewa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...