Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma
MRADI
wa Kilimo Himilivu cha Mtama(CSA) kinachosomamiwa na Shirika la Mpango
wa Chakula Duniani ( WFP)umekuwa chachu ya maendeleo kwa wakulima wa zao
hilo kwenye Wilaya sita za Mkoa wa Dodoma.
Kwa mujibu wa WFP ni
kwamba kupitia mradi huo wakulima hao wanevuna na kuuza mtama tani 28000
wenye thamani ya Sh.bilioni 13 5 kwa msimu wa Kilimo wa mwaka
2020/2021.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma ,Mkuu
wa Ofisi Ndogo ya WFP Neema Sitta amesema mradi huo umeleta tija kubwa
kwa wakulima ambao kwa Sasa mbali ya kuvuna mtama mwingi pia wamekuwa na
soko la uhakika ,hivyo hakuna changamoto ya kukosa soko kwani lipo la
uhakika.
"Mradi wa CSA unatekelezwa katika vijjji zaidi ya 200
vilivyopo kwenye wilaya sita za Mpwapwa,Chamwino, Bahi, Kongwa, Chemba
na Kondoa ambapo kwa msimu wa mwaka 2020 hadi 2021 wamefanikiwa kuuza
zaidi ya tani 28,000 za mtama, zenye thamani ya Sh. bilioni 13.5.
"Wanaofadhili
mradi huu ni Shirika la Maendeleo ya Ireland (IrishAid) na kusimamiwa
na WFP lakini wanaoutekeleza ni FarmAfrica kwa Sh.bilioni 1.7.Uzuri wa
mradi huu umegusa wakulima 22,000 na kunufaisha zaidi ya watu
100,000,"amesema.
Aidha Sitta amesema matarajio yao ni kuona
wakulima wa mtama wanaongeza uzalishaji katika msimu huu mpya wa kilimo
na WFP wako tayari katika kuhakikisha wanashirikiana kikamilifu na
wakulima hao wa mtama.Sababu ya kuamua kujikita katika kilimo cha mtama
ni kutokana na zao hilo kukubali kwenye ardhi na mazingira ya Dodoma,
pamoja na uhakika wa soko".
Amefafanua soko kubwa la zao la
Mtama kwa hapa nchini linahusisha wanunuzi wakubwa na miongoni mwao ni
Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) na kampuni nyingine za ndani na nje ya
nchi.Pia kuna soko la Mtama mweupe Sudani Kusini.
"WFP na
FarmAfrika kupitia nradi wa kilimo himilivu tumeweza kuunganisha
wakulima na kubwa zaidi kuwa na soko la uhakika na kwa sasa bei ya zao
la mtama kilo moja inaunzwa Sh.550 kutoka Sh. 250 ya awali ,"amesema.
Kwa
upande wa Meneja Mradi wa Kilimo Himilivu cha Mtama kutoka Shirika la
FarmAfrica Tanzania Grace Changanyika amefafanua kupitia mradi huo
wakulima wa mtama wamepiga hatua kubwa ya kimaendeleo.
Wakati huo
huo baadhi ya wakulima wa zao hilo wameishukuru WFP na FarmAfrica kwa
kuwapelekea mradi huo ambao umewawezesha hivi kuwa na tofauti kubwa
katika maisha."Kwa sasa hata vipato vyetu, tunavuna mtama kwa wingi
tofauti na hapo nyuma kabla ya kuja kwa mradi huu."
Mmoja ya
wakulima wa zao la Mtama ambao wananufaika na mradi huo akiwemo Patrick
Mbeho ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mkola wilayani Bahi amesema mradi
huo umefanya mapinduzi makubwa kwenye maisha yake,amekuwa na mafanikio
makubwa.
“Kwangu haya ni mapinduzi ya kiuchumi, kijamii na
maendeleo kwani nilikuwa napata Sh. milioni mbili kwa shamba la hekari
20 ila kwa sasa napata hadi Sh. milioni sita na wakati mwingine
Sh.milioni Saba.Nimejenga nyumba ya biashara,pia ninayo mashine ya
kupembulia mtama na mengine mengi,” amesema.
Mwandishi wa Gazeti la Raia Mwema Suleiman Msuya ( kushoto) na Mussa Juma wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewaa na Neema Sitta ambaye ni Mkuu wa Ofisi Ndogo za WFP Dodoma alipokuwa akizungumzia miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na Shirika hilo ukiwemo mradi wa kilimo himilivu cha Mtama kwenye Wilaya sita za Mkoa huo.
Mkuu wa Ofisi Ndogo za Shirika la Mpango wa Chakula Duniani Mkoa wa Dodoma Neema Sitta akizungumza na waandishi wahabari kuhusu majukumu ya Shirika hilo pamoja na miradi mbalimbali wanayoitokea ikiwemo mradi wa kilimo himilivu mtama na mbogamboga.
Mmoja wa wanafaika wa kilimo himilivu cha mtama akiwa akiwa ameshika ungo ukiwa na mtama
Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani ( WFP) Tanzania Desta Laiza akizungumza jambo kwa waandishi wa habari waliyokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Shirika hilo
Muonekano wa shamba la Mtama ambalo linalimwa na mmoja ya wanafuika wa zao la Mtama katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
Baadhi ya waandishi wa habari wakiandika maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkuu wa Ofisi za WFP Mkoa wa Dodoma Neema Sitta.Waandishi hao wako kwenye mkoa huo kwa lengo la kutembelea miradi inayosimamiwa na WFP
Meneja wa Mradi wa Kilimo Himilivu cha Mtama kutoka Shirika la FarmAfrica Grace Changanyika(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi huo.
Wakulima wa zao la Mtama wakihifadhi mtama kwenye chumba maalumu cha kuhifadhia mtama walichokitenga kwenye nyuma yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...