Na.Khadija Seif, Michuzi TV

MFALME wa Muziki wa Bongofleva Ali Saleh Kiba maarufu kama Alikiba ameng'ara  kwenye Tuzo za Muziki nchini zilizofanyika usiku wa kuamkia April 2 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano cha Kimataifa (JNICC) jijini Dar es salaam.

Alikiba ameondoka na Tuzo Tano kupitia Album yake "Only 1 king" aliyoiachia mwishoni mwa mwaka 2021.

Alikiba ,ameshinda katika kipengele Cha Album bora, Msanii Bora wakiume wa Mwaka,Mtunzi Bora wa Mashairi, video Bora ya mwaka, , Mwanamuziki bora chaguo la watu.

Hata hivyo Alikiba hakuweza kuhudhuria katika kilele cha tuzo hizo badala yake wawakilishi wake waliweza kuzipokea tuzo na kuwashukuru watanzania Kwa kumpigia kura nyingi za kishindo.

Wawakilishi kutoka kundi la "Kings Music" wakipokea tuzo ya Msanii wa Muziki nchini Alikiba mara baada ya kushinda katika tuzo za Muziki zilizofanyika usiku wa April 2 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa  Kimataifa JNICC Jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...