Na Janeth Raphael, Michuzi Tv

Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda Leo April 11,2022,amesema kuwa Mfumo wa Elimu nchini unahitaji maboresho zaidi ili kuleta maegeuzi kwa Taifa na kuhakikisha vijana wanapomaliza shule wawe na uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa.

Waziri Mkenda ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, amewasihi kupitia upya Mfumo mzima wa Elimu pamoja na Sera zake ikiwemo Mitaala yake ili kuhakikisha Taifa linanufaika na wataalamu wanaotokana na Elimu hapa nchini. 

Aidha Prof.Mkenda amezungumzia ubora wa Elimu inayopatikana Nchini kuanzia Msingi hadi Vyuo kuwa unapaswa kupitiwa ili kumuandaa kijana kuwa mtaalamu wa kile alichokisomea huku akisema Mifumo ya Elimu haijakamilika ndio maana kuna baadhi ya vijana wanamalizi hadi vyuo vikuu lakini bado hawakidhi katika taaluma walizosomea. 

"Tunahitaji kuandaa Mtaala uliokamilika,Embu tujiulize sote hapa kwa nini wataalamu wetu sio wazuri?,kwa sababu elimu yetu haijakamilika haimuandai kijana katika viwango vinavyotakiwa ndio maana nawaambia kuna haja ya kupitia upya Sera na mfumo wa elimu yetu,"Amesema Waziri Mkenda na kuongeza kuwa 

"Tuna wajibu wa kutoa wataalamu wenye Ubora na sio wataalamu wengi wasio na Ubora niwaambie tu ni vigumu sana Watanzania kufaidika na matunda ya wataalamu wetu kwa sababu ya mfumo wa Elimu yetu kwa sasa," alimaliza Prof.Mkenda 

Kwa upande Mwingine Mwenyekiti wa Baraza hilo Ambaye pia ni katibu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Eliamani Sedoyeka amesema kuwa Baraza hilo lipo tayari katika kuhakikisha taratibu za Wafanyakazi na taratibu za uandaaji wa Rasimu ya Bajeti ya mwaka 2022/2023 ya wizara hiyo inaenda kujikita katika kuwekeza kwenye maboresho ya elimu lengo likiwa ni kuwatengeneza wataalamu wenye ubora kwa ajili ya kuwasaidia watanzania. 

Pia Katibu wa CWT Deus G. Seif amesema yakuwa bila kuwa na walimu wenye ubora katika Shule zetu tutaendelea kuzalisha watalaamu wasio na vigezo hivyo ni vyema kuhakikisha wanaotoa elimu iwe na vigezo vya kutosha ili kusaidia hii Taaluma inayotegemewa na Taifa. 

Deus Seif amesema "Nataka niwahakikishie mwalimu akikosea gharama yake ni kubwa sana kuliko kosa kufanywa na daktari au Mhandisi kwa sababu unaweza kulirekebisha lakini kosa la Mwalimu ni hatari sana."

Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...