Na Pamela Mollel,Arusha
Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia vijinini Camartec imebuni jiko linalotumia miale ya jua katika matumizi yake ya kupika vyakula mbalimbali kwa lengo la kuwawezesha wananchi kuendelea kutunza mazingira na kubana matumizi
Akizungumza hivi karibuni jijini Arusha Kaimu mzalishaji Mhandisi, Boniface Masawe wakati wa ziara ya waandishi wa habari pamoja na watafiti iliyofadhiliwa na COSTECH waliofika katika eneo hilo kwa lengo la kujifunza na kuandika habari za Sayansi na Teknolojia, alisema jiko hilo ni mfumo wa jua na nimahususi kwa vyakula vya kuchemsha
Alisema kuwa jiko hilo linauwezo wa kupika vyakula mbalimbali kama nyama,maharage,makande na vyakula vingine isipokuwa vya kukaanga
Mhandisi Masawe alisema jiko hilo ni rafiki kabisa na mazingira kwa namna ambavyo limetengenezwa na halitumii kuni wala mkaa wakati wa kuwasha bali hutumia miale ya jua tu
"Katika kutunza mazingira jiko hili linapunguza matumizi makubwa ya kuni na mkaa kutokana na
namna lilivyotengenezwa"alisema Masawe
"Maisha yamekuwa magumu sana kuna wakati mtu unashindwa kumudu kununua kuni,mkaa au gesi lakini kwa jiko hili unachohitaji zaidi ni jua tu"alisema Masawe
Pia aliwataka wananchi kutunza mazingira ili kulinda viumbe hai pamoja na binadamu kuendelea kuishi katika mazingira safi na salama
Alisema kinachofurahisha zaidi katika jiko hilo ni namna ambavyo linabana matumizi na kuokoa muda wakati wa utumiaji ukilinganisha na majiko mengine
"Hili jiko sifa yake kubwa ni kupika kwa muda mfupi mno,mfano ukipika maharage ndani ya dakika 45 yameiva lakini mkaa au kuni lisaa limoja hadi mawili kuchemsha maharage au makande"alisema Mhandisi Masawe
Aidha alisema kuwa jiko hilo linadumu zaidi ya miaka 20 na linaendelea kutumika bila kubadilisha kitu chochote zaidi ya kufanyia usafi
Jiko hili lilibuniwa na kituo hicho toka mwaka 1999 na mwaka 2000 lilianza kutumika rasmi hapa Tanzania
Kaimu mzalishaji Mhandisi Boniface Masawe akionyesha jiko walilobuni jijini Arusha,linalotumia miale ya jua kwa waandishi wa habari waliofika katika kituo hicho cha Camartec kwa lengo la kujifunza na kuandika habari za Sayansi na Teknolojia Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...