Na Farida Mangube ,Michuzi TV Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martin Shigela  amelitakashirika la ugavi wa Umeme Tanzania Mkoa wa Morogoro (TANESCO) kuhakikisha linaongeza kasi ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ifakara ili kukipunguzia mzigo Kituo cha kupoza umeme cha Msamvu.

Shigela ameyasema hayo kutokana na kituo cha Msamvu  kupata hitilafu ya  tangu tukio la kituo hicho kuwaka moto Mwezi Agasti  mwaka jana

Shigela metoa rai hiyo baada ya   moja ya transfoma  kubwa katika kituo cha Msamvu Manispaa ya Morogoro leo majira ya mchana kupata hitilafu na kuwaka moto.

Shigela amesema Transforma iliyopata hitilafu na kuwaka moto  ni moja na kwamba ililetwa baada ya tukio la moto la mwaka jana huku chumba cha kuendesha mitambo kituoni hapo.

Amesema chumba cha mitambo   hakikuungua katika tukio ndicho kimewaka moto, ndipo akatoa rai kwa TANESCO kufanya jitihada za makusudi kudhibiti kutokea kwa ajali ya moto mara kwa mara katika kituo hicho..

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Mhandisi Fedgrace Shuma amesema kwasasa bado wataalamu wanafanya tathimini kubaini kiwango cha madhara yaliyojitokeza pamoja na kufanya jitihada za kurejesha huduma ya umeme katika maeneo  yaliyoathirika.

Maeneo yaliyo athirika kutokana na hitilafu hiyo ni maeneo yote ya mji wa Morogoro na kwamba huduma ya umeme itarejea kupitia kituo cha umeme cha Chalinze.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...