*Yatoa mafunzo ya usalama wakati majanga kwa wafanyakazi waliomstari mbele

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Wakala wa  Mabasi Yaendayo  Haraka (DART) umesema kuwa  wanaendelea na maboresho mbalimbali ili kuweza kuendana na viwango vya kimataifa katika sekta ya usafirishaji wa abiria ardhini.

Hayo ameyasema Mkuregenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa DART Deus Kasmir wakati akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji katika ufunguzi wa mafunzo ya usalama wa huduma kwa wafanyakazi walio mstari mbele pindi ajali ikitokea wanawezaje  kutoa huduma yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Deus amesema kuwa DART imejipanga katika kutoa huduma ili bora ya usafirishaji wa abiria ndio maana imeelekeza kutoa mafunzo katika kukidhi viwango vinavyoendana na usafirishaji huo.

Amesema sekta ya usafirishaji ni muhimu katika uchumi katika kumuondoa mtu mmoja kupeleka sehemu nyingine ili aweze kuzalisha kwa muda mwafaka.

Aidha amesema mafunzo wanayoyatoa ni kwenda na jitihada za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa na usafiri bora na salama.

"DART tumejipanga kwenda kutoa viwango vya kimataifa ya usafirishaji wa abiria  ambapo kila mwananchi aweze kufurahia huduma hizo na hata watu wengine kutoka mataifa waje kujifunza huduma zetu"amesema Kasmir.

Aidha amesema kuwa mafunzo ya usalama ni muhimu wakati kunakuwa kumetokea ajali watu waweze kujua sehemu ya kuanzia ikiwemo kutoa huduma ya kwanza na wao kutambua namna ya kuweza kujiepusha na madhara wakati kutoa huduma hizo.

Mkurugenzi wa Shirika la Hesafee Tanzania Dk.Amini Mshana amesema Shirika hilo lipo kwa ajili ya huduma za Menejimenti ya majanga mbalimbali na namna ya kuweza kuyakabili.

Amesema watu wengi katika utoaji wa huduma lazima wawe na mafunzo ya kuweza kuyakabili majanga ikiwemo kutoa huduma ya kwanza pale inapotokea

Amesema  wafanyakazi wa DART waliombele kuwa na mafunzo ya usalama kutasaidia pale inapotokea kujua mambo gani yanatakiwa pamoja na kuangalia usalama katika eneo husika.

Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Deus Kasmir  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya usalama kwa wafanyakazi waliomstari mbele namna wanavyoweza kutoa huduma wakati majanga,jijini Dar es Salaam.
Mkurugezi wa Shirika la Hesafee Tanzania Dk.Amini Mshana akitoa mafunzo ya namna ya watoa huduma waliomstari wa mbele wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) wanavyoweza kushiriki wakati wa majanga ,jijini Dar es Salaam.

Picha  hii namna ya ajali ikiwa imetokea na wahusika wanavyoweza kukabiliana kwa huduma zote za utoaji wa majeruhi ,walifariki na usalama wa eneo husika wakati wa mafunzo ya usalama jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala ,Usimamizi wa Rasilimali Watu na Mawasiliano Dk.Eliphas Mollel akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo ya usalama wakati wa ajali yaliyotolewa na Shirika la Hesafee Tanzania ,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo ya usalama kwa wafanyakazi wa DART ,jijini Dar es Salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...