Na WAF - DODOMA.

Wataalam katika Sekta ya Afya wametakiwa kuongeza maarifa kupitia Moduli ya Elimu Mtandaoni ili kuboresha usimamizi wa Mnyororo wa Bidhaa za Dawa pamoja na kuipunguzia Serikali gharama kwenye eneo la mafunzo.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale leo alipokuwa akizindua Moduli ya Elimu Mtandanoni (E-Learning leo Jijini Dodoma

"Moduli hii ya imeundwa ili kuboresha ujuzi na ufanisi kwa watumishi walio katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuongeza uwezo wao katika kufanya maamuzi sahihi kwenye usimamizi wa bidhaa za afya" amesema Dkt. Sichwale.

Dkt. Sichwale amesema kuwa kupitia mafunzo katika Moduli hiyo, itaipunguzia Serikali gharama katika eneo la mafunzo na kwa mtumishi katika kujiendeleza na kupata alama za kumwezesha kuhuisha usajili wake kitaaluma (CPD)

"Kupitia moduli hizi Serikali imeweza tumesogeza zaidi elimu ya maswala ya mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa watumishi wetu na sasa mtumishi ataweza jifunza akiwa popote hapa nchini" amefafanua Dkt. Sichwale

Dkt. Sichwale ametaja baadhi ya masomo ambayo yatakuwa yabapatikana kwenye Moduli hiyo yakiwemo; Bottom up Quantification, Supply Chain Key Performance Indicators, Health Commodities Revolving Fund Guideline, Electronic Logistics Management Information System (e-LMIS) pamoja na Data Analytics.

"Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo tutaendelea na mpango wa kuongeza moduli nyingine zaidi mfano katika eneo la matumizi sahihi ya dawa, mwongozo wa matibabu nchini, utunzaji sahihi wa bidhaa za afya na maswala ya uongozi na usimamizi wa shughuli za afya" amesema Dkt. Sichwale.

Ili kuweza kupata elimu kwa njia ya mtandao watumishi wa afya wanatakiwa kuingia kwenye kompyuta au simu janja yenye mtandao na kufungua tovuti http://elearning.moh.go.tz na kujisajili ili kuweza kupata mafunzo.

Naye Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi amesema kuwa lengo la elimu mtandaoni ni kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazopatika katika mnyororo wa bidhaa za afya nchini.

Kwa upande wake Msajili wa Wataalam wa Maabara, Bi. Mary Mtui amesema kuwa fursa hii ya kuwa na moduli mtandao wataitumia vema ili kuhakikisha inaleta tija katika utendaji kazi wa wataalamu wao nchini.

Naye Kaimu Naibu Msajili, Bw. Godfrey Ngonela akitoa neno la shukrani ametoa wito kwa wataalamu wa afya kutumia moduli hizo katika kuwahudumia wananchi ili kuleta uwajibikaji sahihi katika sekta ya afya na ufanisi kazini.

Wataalam wakiwa kwenye uzinduzi wa Moduli ya Elimu ya Mtandao ya usimamizi wa bidhaa za afya



Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale akisema jambo kwenye Uzinduzi wa Moduli ya Elimu ya Mtandao ya usimamizi wa bidhaa za afya
Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daud Msasi akisema jambo kwenye uzinduzi wa Moduli ya Elimu ya Mtandao ya usimamizi wa bidhaa za afya
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...