Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib, amesema ni vyema kwa wajasiriamali kujiwekea mikakati imara katika kukuza biashara kwa maendeleo ya Taifa.

Mama Zainab ameyasema hayo Aprili 20, Gando- Mabaoni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika muendelezo wa Ziara yake Kisiwani humo ambapo ametembelea Vikundi mbali mbali vya Wajasiriamali na kuzungumza nao kuhusu biashara zao na pia Changamoto zinazowakabili.

Mama Zainab amesema vikundi vya ujasiriamali vinapaswa kusajiliwa na kufuata taratibu zote zinazohitajika ili kuviwezesha kutambulika kisheria na kusaidilika pindipo zikitokea fursa muhimu zikiwemo za ufadhili.

“Lengo letu ni kuona kwa kiasi gani vikundi vyote vinakuwa imara na kujiendesha ili hatimaye kufanikisha lengo la kumkomboa Mwanamke na jamii kwa ujumla ”, amesema Mama Zainab.

Aidha Mama Zainab amesisitiza kuwa wajasiriamali wanapaswa kupatiwa elimu stahiki ya namna bora ya kukuza bidhaa zao ili kuongeza tija katika soko la biashara.

Kwa nyakati tofauti, wajasiriamali hao walipata fursa ya kutoa shukrani zao za dhati kwa Mama Zainab, kutokana na kile walichotaja kuwa ni juhudi za kipekee za kuwafikia ili kujionea shughuli wanazozifanya sambamba na kuwashauri juu ya namna bora za kutatua changamoto zinazowakabili.

Katika ziara hiyo Mama Zainab ametembelea wajasiriamali wa Bopwe, Kinyasini mabondeni, Chwale na Kitambuu, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.



Mke wa Makamu wa kwanza wa Rais Mama Zainab Kombo Shaib, Aprili 20, ametembelea mradi wa kilimo cha mboga mboga na matunda kilichopo katika Kijiji cha Bopwe,wilaya ya Wete,Mkoa wa kaskazini Pemba.
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib (kulia) Aprili 20, akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa kikundi cha ujasiriamali wa Mwani Ndugu Hamadi Juma Mussa (kushoto), Katika kijiji cha Kitambuu,wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
`Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib,Aprili 20, akizungumza na wajasariamali alipotembelea mradi wa ufugaji wa kuku,katika kijiji cha Kambini-Kojani Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...