Hayo alisema Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB) Dkt.Fatma R.Khalfan wakati wa Uzinduzi wa Klabu ya haki za binadamu na utawala bora katika Kongamano la kumbukizi ya Hayati Abeid Amani Karume, Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lililoandaliwa na Umoja wa Klabu zilizopo katika  Chuo cha Mipango Aprili 7,2022.
 
Dkt. Fatma alielezea jitihada kubwa zilizofanywa na Hayati Abeid Amani Karume katika kuleta usawa na kuinua heshima na utu wa wananchi wa Zanzibar. 
Kwa upande wa kuitambulisha Tume Dkt Fatma  alisema kuwa Ibara ya 129 mpaka 131 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imeelezea Tume ikiwemo majukumu yake moja wapo kuwa ni  kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya  haki za binadamu na misingi ya utawala bora, kupokea malalamiko, kufanya uchunguzi na utafiti kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora kama ikitokea uvunjifu wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kukiukwa. Sambamba na utoaji wa mapendekezo katika sheria mbalimbali zinazosimamia maswala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
‘Tume ina majukumu mengi hayo ni baadhi ya majukumu ambayo nimeyataja ili muweze kufahamu kwa ufupi’. Alisema Dkt. Fatma
 
Aidha, Dkt. Fatma alielezea kuwa Tume imeingia mkataba  wa mashirikiano na asasi za kiraia 21 katika kutoa kusimamia maswala ya haki za binadamu.
‘Asasi hizi za kiraia zinashirikiana na Tume katika kutoa elimu ya masuala ya haki za binadamu ’’Alisema Dkt. Fatma.
Kwa upande wake Bw. James Kalulu, Mratibu wa Umoja wa Klabu hizo alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kushirikiana na kutafakari mambo mazuri yaliyofanywa na mzee wetu Hayati Abeid  Amani Karume sambamba na kuhamasisha vijana  kushiriki kwa dhati kwenye shuguhuli za kizalendo na kujenga Taifa bora.
Bw. Kalulu alioa shukrani kwa Tume kwakutoa uelewa wa pamoja kuhusu Tume ya haki za binadamu na Utawala Bora pamoja na kuzindua Klabu ya haki za binadamu.
‘Awali nilikua nafikiri Tume hii ni taasisi isiyoyakiserikali kupitia maelezo ya Kamishna nimepata kuielewa vizuri zaidi,Tunashukuru’’ alisema Kalulu.
 
 Uzinduzi wa Klabu ya haki za binadamu katika  Chuo  hiko  ni moja ya mikakati ya Tume kuanzisha Klabu katika zoezi la kuanzisha Klabu katika Taasisi za elimu kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vya  elimu ya juu nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...