Na. Angela Msimbira KONGWA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde ameziagiza Halmashauri zote nchini zilizopatiwa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari za wasichana kuandika taarifa ya kina kuhusu maendeleo ya ujenzi wa shule hizo na kuziwasilisha Ofisi ya Rais – TAMISEMI ndani ya siku saba.

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kibaigwa leo tarehe 5 Aprili, 2022 Mhe. Silinde amesema kuwa Halmashauri hizo zinatakiwa kuleta taarifa ya kina inayoonyesha matumizi ya dhamani ya fedha iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule hizo.

Mhe. Silinde amesema kuwa jumla ya shule za wasichana 15 zinajengwa katika Halmashauri nchi nzima ambapo kila shule ilipelekewa kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa Shule hizo. 


Akikagua Maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaigwa Mhe. Silinde amesema hakuridhishwa na ubora wa majengo yaliyojengwa katika shule hiyo, matumizi ya fedha zilizotumika katika ujenzi huo na dhamani ya fedha zilizotumika kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ambayo hadi sasa haijakamilika..

"Sijaridhishwa na Ujenzi wa shule hii kwa kuwa majengo yanaonekana kwa nje yamekamilika lakini ndani hayajakamilika, ujenzi wa majengo hauridhishi kabisa, hii ni hujuma ya kutaka kuwaonyesha wananchi kuwa Serikali haikamilishi miradi yake kwa wakati" amesema Mhe. Silinde

Mhe. Silinde amesema kuwa hatasita kuwachukulia hatua wale wote amabao watashindwa kukamilisha ujenzi wa shule za Sekondari za wasichana kwa wakati kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha elimu bora inatolewa katika mazingira bora.
Aidha, Mhe. Silinde amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuhakikisha wanatafuta fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa shule hiyo kwa kuwa Serikali haipo tayari kutoa kiasi cha shilingi bilioni 464.5.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Mkulo ameeleza kuwa kiasi cha shilingi milioni 464.5 zinahitajika kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa shule hiyo ambayo hadi sasa imefika asilimi 68. 14 ujenzi na fedha iliyotumika ni shilingi milioni 993.8.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...