Na Janeth Raphael -Dodoma
Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Charles Kichere amesema kuwa kupitia Ofisi yake ilibaini miamala 17 yenye jumla ya Lita Milioni 31.12 za mafuta zenye makadirio ya ushuru wa forodha shilingi Bilioni 2.89 ambayo hayakuainishwa kama ni Kwa matumizi ya ndani au kusafirishwa kwenda Nchi jirani.
Kichere ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ambapo amesema kuwa hiyo inaashiria kwamba mafuta hayo yalitumika nchini na yalipaswa kutozwa ushuru wa forodha shilingi Bilioni 2.89.
"Ninapendekeza kwamba Serikali iimarishe mifumo ya Udhibiti na usimamizi wa mafuta yanayoingia nchini ili kuzuia matumizi ya mafuta hayo bila Kodi stahiki kulipwa" - Kichere
"Mafuta yaliyopitiliza muda wa kukaa nchini ambayo yalipaswa kwenda Nchi jirani yenye ushuru wa forodha shilingi Bilioni 1.78," Amesema Kichere
Aidha amesema kuwa Lita 2.63 za mafuta zenye makadirio ya Kodi ya shilingi Bilioni 1.78 ziliingizwa nchini kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Nchi jirani,hata hivyo mafuta hayo hayakusafirishwa kwenda Nchi husika kwa zaidi ya miezi 12 kinyume na Sheria ya forodha inayotaka yasafirishwe ndani ya siku 30.
Amesema Kwa mujibu wa sheria za forodha mafuta yanatokana nchini kwa zaidi ya muda uliopangwa yanapaswa kurasimishwa Kwa matumizi ya ndani na hivyo kutozwa ushuru unaotakiwa.
"Ninapendekeza kwamba Serikali iimarishe mifumo ya Udhibiti na usimamizi wa mafuta hayo nchini bila Kodi stahiki kulipwa,pia mamlaka ikusanye ushuru wa forodha wa shilingi Bilioni 1.78 kwenye Lita Milioni 2.63 pamoja na adhabu kwa mafuta ambayo hayakuondoshwa nchini,"alisema.
Aliendelea kusema kuwa mizigo iliyokaa muda mrefu kwenye maghala yenye dhamana ya forodha kiasi Cha shilingi 1.08 bila kuingiza kwenye mnada.
Maghala Saba yenye dhamana ya forodha(bonded warehouses)yalikuwa na mizigo yenye dhamana ya shilingi Bilioni 1.08 iliyokaa muda muda mrefu bila kuingiza mnadani Wala kuombewa nyongeza ya muda kama sheria inavyotaka.
Amesema bidhaa kukaa muda mrefu katika maghala yenye dhamana bila kuingiza mnadani kunaizuia Serikali kikusanya Kodi na ushuru kwa wakati.
"Ninapendekeza kwamba Serikali ifanye mnada wa bidhaa zote zilizokaa muda mrefu kwenye maghala yenye dhamana ya forodha Kwa mujibu wa taratibu na sheria,"amesema.
Kwa upande mwingine Kichere alitoa ufafanuzi kuhusu mwenendo wa mashirika mawili ambayo ni kampuni ya ndege Tanzania na kampuni ya mkulazi.
"Mwenendo wa kampuni ya ndege Tanzania umeimarika ukilinganisha na mwaka uliopota kwa sababu kwa mwaka 2020/21 kampuni iliongeza mapato kwa asilimia 11 na kupunguza matumizi kw asilimia tatu,kampuni ilipunguza hasara ya jumla kutoka shilingi Bilioni 60.25 mwaka 2019/20 Hadi kufikia shilingi 36.18 mwaka 2020/21,"- Kichere
Amesema kuwa Kampuni ya mkulazi imekuwa ikipata hasara kwa miaka mitano mfululizo tangu mwaka wa fedha 2016/17 hadi tarehe 30 Juni 2021 kampuni ilikuwa na limbikizo la hasara ya shilingi Bilioni 17.10.
"Hasara hiyo ilisababishwa na ucheleweshaji wa kuanza uzalishaji wa sukari Kutokana na kuchelewa kufunga mitambo ya uzalishaji,mwenendo huu wa hasara unapunguza mtaji wa kampuni," - Kichere
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...