Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Samia Suluhu Hassan amewasilisha jina la Abdulrhaman Kinana kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho ili wampitishe kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.
Akizungumza mbele ya wajumbe hao leo Aprili 1,2022 , Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kwamba wamependekeza jina hilo baada ya Mzee Phillip Mangula aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kuamua kung'atuka kwenye nafasi hiyo
Rais Samia amesema kwamba Mangulla amekitumikia Chama hicho kwa muda mrefu na amekuwa akikitumikia Chama tangu mwaka 1962 ambapo wakati huo yeye( Rais Samia) alikuwa na umri wa miaka miwili.
"Ajenda hii imekuja na chimbuko Mzee Mangulla ambaye tumemtumia muda mrefu na sasa ameamua kupumzika, amewasilisha barua ambayo nitaisoma mbele yenu,"amesema Rais Samia wakati akitoa sababu za kwanini wamependekeza jina la Kinana kwenye kuchukua nafasi hiyo.
Ameongeza kuwa barua ya Mzee Makamba ameipeleka kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa inayoeleza kung'atuka nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara na ametoa sababu mbalimbali na kubwa ni ya umri kwani Jana Mangulla ametimiza miaka 81."Ameanza utumishi mwaka 1962 na wakati huo Mwenyekiti wenu nikiwa na miaka miwili tu.Amekitumia Chama chetu kwa nafasi mbalimbali."
Miongoni mwa nafasi ambazo amezitumikia mzee Mangulla ni pamoja na nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwa miaka 10.Katika barua yake ya kung'atuka mzee Mangula ameeleza kwamba anatoa shukrani za dhati kwa viongozi wa CCM,sekratarieti na Wana CCM kwa ujumla.
Amewahakikishia Wana CCM kuwa ataendelea kuwa mwanachama mtiifu ,hivyo akamalizia kwa kuomba naomba nafasi hiyo achaguliwe Mwana -CCM mwingine kushika nafasi hiyo
Baada ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum kuwa baada ya barua hiyo Kamati Kuu walikaa na kujadili na kisha jina lake kupelekwa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambayo ikaagiza mapendekezo haya yapelekwe kwa wajumbe hao ambao ndio wenye jukumu la kupitishwa pendekezo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...